Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 02:35

WFP yalazimika kupunguza mgao wa chakula kwa raia milioni 2 wa Afghanistan


Wanawake raia wa Afghanistan wakisubiri kupatiwa msaada katika kituo cha Shirika la Mpango wa Chakula la UN, WFP.
Wanawake raia wa Afghanistan wakisubiri kupatiwa msaada katika kituo cha Shirika la Mpango wa Chakula la UN, WFP.

Shirika la Mpango wa Chakula la UN limelazimika kupunguza mgao wa chakula mwezi huu  kwa raia  milioni 2 wa Afghanistan na limetahadharisha juu ya “janga” la kipindi cha majira ya  baridi.

Shirika hilo limeongeza kuwa iwapo litaishiwa na fedha jamii zilizopo maeneo ya vijijini watapatiwa chakula kidogo, mkurugenzi wa shirika hilo nchini humo alisema.

Kupunguzwa kwa mgao kumekuja wakati kunaongezeko la wasiwasi juu ya kupungua kwa misaada kwa Aghanistan, ambapo mpango wa UN wa kukabiliana na hali ya kibinadamu unapata tu robo ya ufadhili, hata pale bajeti ilipopunguzwa kutokana na uhaba wa fedha.

WFP itaishiwa na ufadhili kwa chakula na msaada fedha taslimu ifikapo mwisho wa mwezi Oktoba na shirika hilo limelazimika kuendelea kukata misaada kipindi cha mwaka huu kwa raia milioni 10 wa Afghanistan.

Usambazaji chakula katika maeneo ambayo yatapoteza mawasiliano wakati wa majira ya baridi umekuwa finyu.

WFP ilisema iwapo hakuna ufadhili utakaopatikana, asilimia 90 ya maeneo ya vijijini yenye uhitaji yatapoteza mawasiliano bila ya kuwa na chakula, na hata maeneo yenye kufikiwa, watu hawatapa mahitaji wakati hali ya hewa itakapokuwa mbaya sana.

“Hilo ni janga ambalo ni lazima tuliepuke,” Mkurugenzi wa WFP nchini Afghanistan Hsiao-Wei Lee aliiambia Reuters.

Robo tatu ya watu nchini Afghanistan wanahitaji misaada ya kibinadamu wakati nchi yo ikiibuka kutoka miongo kadhaa ya vita chini ya utawala wa uongozi wa Taliban uliotengwa kimataifa, uliochukua madaraka kutoka kwa majeshi ya kigeni yaliyokuwa yanaungwa mkono na Marekani baada ya kuondoka nchini mwaka 2021.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG