Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:13

Marufuku ya ulanguzi wa dawa za kulevya Afghanistan, yaleta mafanikio


Kiongozi mkuu wa kundi la Taliban nchini Afghanistan, Jumapili ameweka wazi kwamba kampeni yao dhidi ya uzalishaji haramu wa dawa za kulevya nchini humo imetokomeza kilimo cha mazao ya afyuni ambayo hutumiwa kutengeneza dawa za kulevya kama heroin.

Tamko la Hibatullah Akhundzada, linafuatia ripoti za karibuni za vyombo vya habari na picha za satelaiti zinazoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na Marekani, na kuthibitisha kwamba kilimo cha kila mwaka cha mazao ya afyuni kimepungua kwa kiasi kikubwa kwa taifa ambalo ni mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa mazao hayo.

Upunguzaji huo unatokana na agizo lililotolewa na mkuu wa Taliban, la Aprili 2022, ambalo lilipiga marufuku kabisa kilimo, uzalishaji, matumizi, usafirishaji, na uagizaji wa dawa zote haramu Afghanistan.

Marufuku hiyo iliruhusu vitengo vya kupambana na dawa za kulevya vya Taliban kutokomeza kilimo cha mauwa ya afyuni katika nchi hiyo maskini iliyoharibiwa na vita, ambayo ilichangia asilimia 85 ya uzalishaji duniani mpaka mwaka jana, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG