Hatua hiyo imepelekea mashirika ya misaada kuacha kutoa msaada muhimu kwa mamilioni ya watu.
Mwezi Machi, Umoja wa Mataifa ulizindua Mpango uliokuwa umechelewa wa msaada wa Kibinadamu, au HRP, kwa Afghanistan, ukiomba wafadhili kutoa dola bilioni 4.6 kusaidia zaidi ya Waafghanistanmilioni 23 walio hatarini zaidi mwaka huu. Uzinduzi wa mpango huo ulicheleweshwa kwa miezi miwili kufuatia tangazo la Taliban la mwezi Disemba mwaka jana kupiga marufuku wanawake wa Afghanistan kufanya kazi katika mashirika ya Umoja wa Mataifa.
"Ni sehemu ndogo tu ufadhili huo ulioahidiwa ambayo imepokelewa, na hiyo ndiyo sababu msaada huo umepunguzwa," Richard Hoffman, mkurugenzi wa ACBAR, jukwaa la uratibu wa mashirika yasiyo ya serikali nchini Afghanistan, aliiambia VOA.
Vikwazo vilivyowekewa Taliban vinachangia mzozo wa kibinadamu nchini Afghanistan na "uongozi wa Taliban ndio wa kulaumiwa," Human Rights Watch ilisema Jumanne.
Forum