Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:25

Ugiriki: Manusura 70 wapatiwa msaada baada ya boti iliyosheheni wahamiaji kuzama


Mmoja wa wahamiaji aliyenusurika baada ya boti aliyokuwa akisafiri nayo kuzama.
Mmoja wa wahamiaji aliyenusurika baada ya boti aliyokuwa akisafiri nayo kuzama.

Katika bandari ya Ugiriki ya Kalamata karibu manusura 70 waliokuwa wamechoka walipata msaada baada ya boti ya wavuvi iliyojaa wahamiaji waliokuwa wakijaribu kufika ulaya kupinduka na kuzama baharini Jumatano , maafisa wamesema.

Walikuwa wamelala kwenye mifuko na mablanketi yaliyotolewa na waokoaji katika ghala kubwa ambako wahudumu wa afya waliweka mahema nje kwa ajili ya yoyote anayehitaji huduma ya kwanza.

Kundi la waokozi waliwaokoa abiria 104 wakiwemo kutoka Misri, Syria, Pakistan, Afghanistan na Palestina,

Boti ambayo ilikuwa imesheheni wahamiaji iliyozama nje ya pwani ya Ugiriki Jumatano.
Boti ambayo ilikuwa imesheheni wahamiaji iliyozama nje ya pwani ya Ugiriki Jumatano.

Lakini maafisa wa usalama wanahofia mamia ya watu wengine wanaweza kuwa wamekwama chini ya boti.

Takriban miili 78 imepatikana, na maafisa walibadilisha baadae idadi ya awali ya 79 kufuatia zoezi la kuhesabu miili lililofanyika usiku kucha .

Taarifa ya walinzi wa pwani imesema juhudi zake na meli za uokozi zilikataliwa mara kwa mara, huku watu waliokuwemo wakisisitiza wanataka kuendelea na safari ya Italia.

Forum

XS
SM
MD
LG