Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:55

Viongozi wa Taliban wanapinga tathmini ya UN kwamba wana mgogoro ndani ya kundi


Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid. Feb. 27, 2022.
Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid. Feb. 27, 2022.

Viongozi wa Taliban nchini Afghanistan wamepinga tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa kwamba wanakabiliwa na mapambano ya ndani ya madaraka na kudumisha uhusiano mzuri na makundi ya kigaidi ya kimataifa.

Katika taarifa ambayo msemaji mkuu wa Taliban Zabihullah Mujahid ameshutumu kuwa haina msingi na imejaa chuki ripoti hiyo ambayo timu ya Umoja wa Mataifa ya Uangalizi iliitoa mapema mwezi huu.

Imesema kuwa chini ya kiongozi mkuu Hibatullah Akhundzada, Taliban wamerejea katika sera za kutengwa, zinazozingatia Pashtun, za kiimla za utawala wao wa awali mjini Kabul kuanzia mwaka 1996 hadi 2001. Wa-Taliban wanatoka katika kabila la Pashtun nchini Afghanistan, na wakosoaji wao wanasema makabila mengine hayana uwakilishi katika utawala wao.

Tathmini hiyo ilisema kuwa baadhi ya upinzani unaonekana ndani ya uongozi wa Taliban lakini mamlaka ya Akhundzada yalikuwa yakiongezeka, na ushirikiano katika safu za Taliban huenda ukadumishwa katika kipindi cha mwaka mmoja hadi miwili ijayo.

Forum

XS
SM
MD
LG