Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:44

WFP yaeleza watu 950,000 Msumbiji wanahitaji msaada wa haraka


FILE - Watu waliolazimika kukimbia makazi yao huko mjini Pemba, Mozambique, April 2, 2021 wakisubiri msaada wa kibinadamu.
FILE - Watu waliolazimika kukimbia makazi yao huko mjini Pemba, Mozambique, April 2, 2021 wakisubiri msaada wa kibinadamu.

Shirika la chakula duniani (WFP) linasema zaidi ya watu 950,000 katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji linalokumbwa na uasi wa wanamgambo wanahitaji msaada wa haraka wa chakula.

Watu 50,000 walikimbia makazi yao kufuatia uvamizi wa siku 5 wa mji wa Palma uliofanywa na waasi mapema Aprili.

Hivyo uvamizi huo ulisababisha kuongezaka kwa idadi ya waliyohama makazi yao na wanaokabiliwa na njaa.

Wengi miongoni mwa waliyohama makazi yao wanahudumiwa na familia nyingine ambazo tayari ni maskini.

Familia hizo za wenyeji nazo pia zinakabiliwa na njaa, wafanyakazi wa misaada wamesema.

Watoto ndio wanaathiriwa zaidi na viwango vya juu ya utapia mlo.

Asilimia 21 ya watoto wa chini ya miaka mitano na asilimia 18 ya watoto wa familia za wenyeji wana uzani wa chini, kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na shirika la UNICEF na WFP.

XS
SM
MD
LG