Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:06

Jeshi la Msumbiji limewaua wanamgambo 36


Mfanyakazi wa Shirika la Chakula Duniani, WFP, na watu waliolazimika kukimbia makazi yao wakisubiri maelekezo ya utaratibu wa kupatiwa Chakula huko Cabo Delgado. Picha hii imepigwa Aprili 5, 2021.
Mfanyakazi wa Shirika la Chakula Duniani, WFP, na watu waliolazimika kukimbia makazi yao wakisubiri maelekezo ya utaratibu wa kupatiwa Chakula huko Cabo Delgado. Picha hii imepigwa Aprili 5, 2021.

Mamlaka nchini Msumbiji zimesema Jumamosi wanajeshi wamefanikiwa kuwaua washukiwa wanamgambo 36, wakati wa operesheni ya usalama mjini Palma.

Mji huo wa pwani ulilengwa na wana jihadi wiki mbili zilizopita. Brigadia Chongo Vidigal, msemaji wa jeshi ambaye alizungumza na wanahabari Ijumaa jioni amesema kuwa idadi ya waliouawa huenda ikawa kubwa zaidi.

Vidigal amesema serikali inaamini kwamba jeshi kuingilia kati huko Palma kumekuwa na mafanikio.

Wanamgambo wenye uhusiano na Islamic State wameshambulia mji wa pwani wa kaskazini mashariki wa Palma March 24, na kuharibu majengo na kuwakata vichwa raia.

Wanamgambo hao ambao wanajulikana kama al-Shabaab hawana uhusiano na kundi kama hilo nchini Somalia.

Wanamgambo hao wa Cabo Delgado wamefanya mlolongo wa uvamizI kwenye miji na vijiji ikiwa ni juhudi ya kusimika ukhalifa wa Kiislamu. Bado haiko bayana raia wangapi wameuawa.

XS
SM
MD
LG