Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:48

Watu 48 wafariki katika ajali ya treni ya abiria Taiwan


Waokoaji wakiuhamisha mwili katika kituo cha treni cha Xincheng baada ya mabehewa kuacha njia ya treni kwenye handaki lililoko kaskazini ya Hualien,Taiwan, Aprili 2, 2021. REUTERS/Annabelle Chih
Waokoaji wakiuhamisha mwili katika kituo cha treni cha Xincheng baada ya mabehewa kuacha njia ya treni kwenye handaki lililoko kaskazini ya Hualien,Taiwan, Aprili 2, 2021. REUTERS/Annabelle Chih

Takriban watu 48 wamefariki, na darzeni za wengine kujeruhiwa katika kisiwa cha Taiwan, baada ya treni waliokuwa wakisafiri nayo, kugongana na gari, ambalo lilikuwa limeteleza na kuingia kwenye njia ya treni hiyo.

Maafisa wanasema kuwa, kufuatia ajali hiyo, treni hiyo iliondoka kwenye reli na kupinduka mara kadhaa.

Treni hiyo, iliyokuwa imebeba takriban abiria 500. Waokoaji walionekana wakitafuta manusura na miili ya watu waliokufa, kutoka katika vifusi vya treni hiyo, ambayo ilikuwa imeharibiwa vibaya.

Baadhi ya abiria walivunja dirisha za treni hiyo na kutoka. Maafisa wamesema kuwa treni hiyo, ambayo ilikuwa inatoka mji mkuu Taipei, kwelekea Taitun, ilikuwa imebeba idadi kubwa ya abiria kuliko inavyoruhusiwa.

Wengi wao, walikuwa wanaenda kwa mapumziko ya wikendi ndefu ya Pasaka. Ajali hiyo, ndiyo mbaya Zaidi, kuwahi kutokea katika historia ya hivi karibuni, ya Taiwan.

XS
SM
MD
LG