Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:17

Jaribio la kuiteka Ikulu ya Rais Niger lafeli


Mohamed Bazoum
Mohamed Bazoum

Hali ya utulivu imerejea kwenye Mji mkuu wa Niger, Niamey, kufuatia milio mikubwa ya risasi karibu na ikulu ya rais, usiku wa kuamkia Jumatano.

Hali hiyo imeripotiwa baada ya kikosi kutoka kitengo cha Jeshi la Angani, kilicho karibu na Ikulu, kujaribu kuteka makazi hayo ya rais.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa maafisa wa idara ya usalama nchini humo.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa washambuliaji hao walishindwa nguvu na maafisa wa kitengo cha ulinzi wa rais, waliotumia silaha nzito.

Vyanzo vingine vitatu, vilivyo omba kutokujulikana, kwa sababu haviruhusiwi kuzungumza na vyombo vya habari, vilieleza.

Hata hivyo, vyanzo hivyo havikusema washambuliaji walikuwa wameenda wapi, au kutoa habari kuhusu ni wapi aliko Rais Mahamane Ousmane, au rais mteule Mohamed Bazoum, ambaye anatarajiwa kuapishwa Ijumaa baada ya ushindi wa uchaguzi uliopingwa na Ousmane.

Milio ya risasi ilianza kusikika majira ya saa tatu asubuhi kwa saa za Niger, na iliendela kwa karibu dakika 30, kulingana na mashahidi waliozungumza na Reuters.

Kufikia saa 4 asubuhi barabara zilikuwa wazi na hali ilionekana kuwa ya kawaida, walisema mashahidi kadhaa.

XS
SM
MD
LG