Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:46

Matokeo ya uchaguzi yaanza kutangazwa Niger, upinzani unadai kuwepo udanganyifu


Mgombea wa uras Mohamed Bazoum akipiga kura
Mgombea wa uras Mohamed Bazoum akipiga kura

Tume huru ya uchaguzi nchini Niger imeendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais na ubunge uliofanyika Jumapili.

Mgombea wa urais kupitia chama kinachotawala Mohamed Bazoum, anaongoza katika hesabu ya kura kufikia sasa, japo hana idadi ya kura ya kutosha kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.

Bazoum ana asilimia 40 ya kura kutoka vituo vya kupigia kura 39 kati ya 266. Mshindani wake wa karibu ambaye ni aliyekuwa rais Mahamane Ousmane, ana asilimia 15. Kuna wagombea wa urais 30.

Bazoum, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani, anatarajiwa kushinda uchaguzi huo na kumrithi rais Mahamadou Issoufou, anayestaafu baada ya kuwa madarakani kwa mihula miwili.

Iwapo Issoufou atamkabidhi madaraka mshindi kwa amani, itakuwa mara ya kwanza kwa kwa viongozi kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani nchini Niger yenye jumla ya watu milioni 23.

Niger imeshuhudia mapinduzi ya kijeshi mara nne tangu ilipopata uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960.

Muungano wa vyama vya upinzani wa CAP-2021, ambao Ousmane ni mwanachama, vimetoa madai ya kufanyika udanganyifu katika hesabu ya kura.

Bila ya kutoa Ushahidi wowote, muungano huo umedai kwamba chama kinachotawala kimefanya udanganyifu.

Waangalizi wa uchaguzi kutoka umoja wa Afrika wamesema kwamba uchaguzi huo umedanyika kwa njia iliyo huru na haki.

Iwapo mshindi hatapatikana moja kwa moja, duru ya pili ya uchaguzi itafanyika mwezi Februari.

XS
SM
MD
LG