Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:58

Wanamgambo wameua watu 100 Niger


Waziri mkuu wa Niger amesema kwamba karibu watu 100 wameuawa katika mashambulizi ya wanamgambo katika vijiji viwili karibu na mpaka na Mali.

Brigi Rafini amesema kwamba watu 70 wameuawa katika Kijiji cha Tchombangou na 30 zaidi kuuawa katika Kijiji cha Zaroum-dareye.

Mashambulizi hayo yametajwa kuwa miongoni mwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea Niger katika siku za hivi karibuni.

Niger inakabiliwa na mapigano ya kijamii na kutoka kwa makundi ya wapiganaji wa kiislamu.

Hakuna kundi limekiri kufanya mashambulizi hayo.

Kulingana na meya wa eneo hilo, Amlou Hassane, waliofanya mashambulizi hayo walitumia usafiri wa pikipiki, na kwamba waligawana katika makundi na kutekeleza mashambulizi kwa wakati mmoja.

Aliyekuwa waziri nchini Niger Issoufou Issaka, amesema kwamba kundi hilo limefanya mashambulizi baada ya wanakijiji kuwauwa wapiganaji wao wawili, japo madai hayo hayajathibitishwa na maafisa wa usalama.

Watu wengine 75 wameachwa na majeraha mabaya na wengine wamepelekwa katika mji wa Niamey, kwa matibabu maalum.

XS
SM
MD
LG