Katika mji wa Darfur Magharibi wa El Geneina, watu kadhaa mashuhuri wameuawa katika siku za hivi karibuni wakati watu wanaojitolea wanahangaika kuzika maiti zilizozagaa mitaani, kundi la wanasheria wanatotetea haki za binaadam la Darfur, ambalo linafuatilia mzozo huo, lilisema katika taarifa.
Vurugu na watu kuyakimbia makazi yao huko Darfur kumeongezeka kwa kasi wakati Jeshi la kawaida na Vikosi vya Msaada wa dharura (RSF) vikiendelea na mapigano katika mji mkuu wa Khartoum na maeneo mengine ya Sudan wakati wa mzozo huo wa kugombea madaraka ambao ulioanza katikati ya mwezi Aprili.
Huko El Geneina, mashuhuda wameripoti mawimbi ya mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa Kiarabu na RSF dhidi ya watu wasio Waarabu wa kabila la Masalit, jamii yenye idadi kubwa zaidi katika jiji hilo, mashumbulizi hayo yamesababisha maelfu ya watu kukimbia na kuvuka mpaka jirani na Chad.
Katika ripoti mpya, Human Rights Watch imerekodi mauaji ya raia wasiopungua 40, yakijumuisha watu wa Masalit wasiopungua 28 walionyongwa katika huko Darfur Magharibi katika mji wa Misteri uliopo kilometa 45 kutoka El Geneina.
Vikosi vya RSF na wanamgambo washirika wa Kiarabu waliuzingira mji huo wa Misterrei asubuhi ya tarehe 28 mwezi Mei, kuingia majumbani na kwenye shule na kuwapiga risasi raia kwa karibu kabla ya kupora na kuchoma sehemu kubwa ya mji huo, Ripoti ya HRW ilisema.
Shirika la Human Rights Watch limesema limetoa matokeo ya uchunguzi wake kwa vikosi vya RSF, lakini hawakujibu. RSF - ambao wengi wa wapiganaji wao wanatoka katika kundi la wanamgambo wa kiarabu la Janjaweed ambao miongo miwili iliyopita wamekuwa wakilaumiwa kwa ukatili wa kikabila katika mzozo wa Darfur - hapo awali lilikanusha kuhusika na mauaji katika eneo hilo, wakisema wanachama wowote watakaobainika kuhusika na unyanyasaji wangewajibishwa.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.
Forum