Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:14

Mapigano yazuka Omdurman, Sudan


Mapigano makali yamezuka tena Jumanne kote Omdurman, sehemu ya magharibi ya mji mkuu wa Sudan, wakati jeshi lilipojaribu kukata njia za kusafirisha vifaa na wapiganaji kuimarisha kikosi cha upinzani cha RSF katika mji huo.  

Jeshi lilianzisha mashambulizi ya anga na mizinga mikubwa, na kulikuwa na mapigano ya ardhini katika maeneo kadhaa ya Omdurman, walioshuhudia walisema.

RSF ilisema jana iliidungua ndege ya kivita, na wakaazi walichapisha picha zilizokuwa zikionyesha marubani wakitoka kwenye ndege.

Hakukuwa na maoni ya moja kwa moja kutoka kwa jeshi. Mzozo kati ya jeshi na wanajeshi wa dharura RSF ulianza Aprili 15, na kusababisha mapigano ya kila siku katika mji mkuu, na kusababisha mauaji ya kikabila katika eneo la magharibi la Darfur, na kutishia kuiingiza Sudan katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu.

RSF ilichukua udhibiti wa maeneo mengi ya mji mkuu na imeleta wapiganaji wa ziada kutoka Darfur na Kordofan.

Forum

XS
SM
MD
LG