Imeeleza inachukua hatua hiyo ili kusaidia maelfu ya watu wanaokimbia mapigano baina ya makundi mawili ya jeshi la Sudan.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema takriban watu laki mbili wamekimbia Chad tangu ghasia zilipoanza April mwaka huu.
Wiki iliyopita pekee, watu elfu 20 wamevuka mpaka kutoka mkoa wa Darfur hadi mpaka wa Chad katika mji wa Adre.
WFP imesema wengi wanawasili wakiwa wamejeruhiwa vibaya. Kuna taarifa kwamba raia wanaokimbia wanalengwa makusudi, kukiwa na dalili za vita vya kikabila katika vurugu hizo.
Mapema shirika la kutetea haki za binadamu- Human Rights watch, lilitoa wito kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kufanya uchunguzi wa uhalifu wa vita uliofanyika mkoa wa Darfur magharibi mwa Sudan, ikiwemo mauaji ya dazani za raia.
Forum