Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:49

Sudan na Iran zinapanga kurejesha haraka uhusiano wake wa kidiplomasia


Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian akiwa mjini Tehran, Iran. Jan. 29, 2023.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian akiwa mjini Tehran, Iran. Jan. 29, 2023.

Sudan ilikata uhusiano wa kidiplomasia na Iran mwaka 2016 kufuatia uvamizi wa ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran

Iran na Sudan zimesema zinapanga kurejesha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi haraka iwezekanavyo baada ya waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian kukutana na kiongozi mwenzake wa Sudan anayekaimu nafasi hiyo Ali Sadeq kwa mara ya kwanza tangu uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ulipovunjika miaka saba iliyopita.

David Monda, mchambuzi wa siasa za kimataifa kutoka New York nchini Marekani anaelezea hatua hii ina maanisha nini katika mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Sudan.

David Monda, mchambuzi wa siasa za kimataifa.m4a
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:11 0:00

Sudan ilikata uhusiano wa kidiplomasia na Iran mwaka 2016 kufuatia uvamizi wa ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran.

Hata hivyo Saudi Arabia na Iran zilikubaliana kuanza tena uhusiano mwezi Machi chini ya makubaliano yaliyojadiliwa na China, na kuongeza matarajio kwamba Tehran na nchi nyingine za Kiarabu zitaanzisha upya uhusiano wa kidiplomasia.

Wakati huo huo Sadeq wa Sudan alinukuliwa akisema makubaliano kati ya Saudi Arabia na Iran yataimarisha usalama na utulivu katika eneo hilo na ulimwengu wa Kiislamu.

Forum

XS
SM
MD
LG