Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:06

Surua yashukiwa kuzuka Sudan


Watoto waliwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani iliyoko al-Suwar, takriban kilomita 15 kaskazini mwa Wad Madani, Juni 22, 2023. Picha na AFP.
Watoto waliwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani iliyoko al-Suwar, takriban kilomita 15 kaskazini mwa Wad Madani, Juni 22, 2023. Picha na AFP.

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka walisema Jumapili kwamba wanashuku kuzuka kwa surua katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan.

Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu limesema watoto 13 wamefariki hivi karibuni katika mlipuko unaoshukiwa kutokea katika kambi iliyoko katika jimbo la White Nile nchini Sudan.

"Kila siku tumekuwa tukipokea watoto ambao wanadhaniwa kuwa ugonjwa wa surua, wengi wakiwa na matatizo mengi ya kiafya," shirika hilo liliandika kwenye mtandao wa Twitter.

Shirila hilo la Madaktari Wasio na Mipaka lina zahanati mbili katika eno la White Nile. Linasema lina zaidi ya wagonjwa 3,000 katika kipindi cha mwezi Juni, na linahitaji "kuongeza misaada, kuzidisha huduma kama vile za chanjo, lishe, makazi, maji na usafi wa mazingira."

Wakati huo huo milipuko iliutikisa tena mji mkuu wa Sudan, Khartoum siku ya Jumatatu wakati jeshi lilipowakusanya na kuwataka raia kuchukua silaha dhidi ya mashambulizi mapya ya mahasimu wao wa RSF.

Sauti za mizinga zilitikisa alfajiri katika eneo la kaskazini magharibi mwa Khartoumnma kusonga mbele kuelekea katikati na mashariki mwa mji huo, mashuhuda waliliambia shirika la habari la AFP.

Mapigano hayo "yalianza saa kumi asubuhi na bado yanaendelea," mkazi mmoja alisema.

Katika Mji mkuu uliokumbwa na vita, mapigano yalipungua kidogo katika kipindi cha saa chache baada ya mapambano makali ya Jumapili kati ya wanajeshi watiifu kwa mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF).

Jeshi lilitangaza Jumatatu kuwa liko tayari "kuwapokea na kuwatayarisha" wapiganaji wa kujitolea, baada ya Burhan wiki iliyopita kuwataka Wasudan "vijana na wale wote wenye uwezo wa kupigana" kujiunga na jeshi.

Raia waliochoshwa na vita kwa kiasi kikubwa wameukataa wito huo, na wakiomba kukomeshwa kwa vita hivyo visivyo na kikomo kati ya Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Daglo.

Mbali na Khartoum, baadhi ya mapigano makali sana yalitokea katika eneo kubwa katika mkoa wa magharibi wa Darfur, ambako Jumapili jioni vikosi vya RSF " viilishambulia kambi ya kijeshi" huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini.

Baadhi ya taarifa ya habari hii zinatoka Shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG