Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 07:39

Mapigano makali yaanza tena punde baada ya sitisho la mapigano kumalizika


Moshi ukifuka katika wilaya ya Bahri huko Khartoum, tarehe 21 Juni 2023, muda mfupi baada ya muda wa usitishwaji wa mapigano kumalizika. Picha na AFP.
Moshi ukifuka katika wilaya ya Bahri huko Khartoum, tarehe 21 Juni 2023, muda mfupi baada ya muda wa usitishwaji wa mapigano kumalizika. Picha na AFP.

Mapigano makali yamezuka kati ya makundi hasimu ya kijeshi katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Sudan siku ya Jumatano, wakati sitisho la mapigano la saa 72 lilipomalizika ambapo baadhi ya riporti zimedai kuwepo kwa ukiukwaji wa makubaliano hayo, mashuhuda walisema.

Muda mfupi kabla ya mapatano kumalizika saa kumi na mbili asubuhi, mapigano yaliripotiwa katika miji yote mitatu inayounda mji mkuu wa Sudan, katika maeneo jirani na makutano ya Mto Nile: Khartoum, Bahri na Omdurman.

Jeshi la Sudan na Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) wamekuwa wakipambana kwa zaidi ya miezi miwili, na kusababisha uharibifu katika mji mkuu huo, pamoja na kusababisha ghasia kubwa katika mkoa wa magharibi wa Darfur na kusababisha zaidi ya watu milioni 2.5 kuyakimbia makazi yao.

Mashuhuda walisema ndege za jeshi zilifanya mashambulizi ya anga huko Bahri na RSF ilijibu mashambulizi hayo. Waliripoti mashambulizi ya mizinga na mapigano makali huko Omdurman na mapigano ya ardhini huko kusini mwa Khartoum.

Wakazi pia waliripoti kuwepo kwa mapigano jirani na kambi ya jeshi katika Jimbo la Kordofan Kusini, ambako kikosi kikubwa cha waasi kimekuwa kikijipanga, kikosi hicho ambacho hakijulikani kinaegemea upande gani kati ya makundi yanayopigana mjini Khartoum.

Sitisho hili lilikuwa la karibuni miongoni mwa makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Saudi Arabia pamoja na Marekani katika mazungumzo yaliyofanyika huko Jeddah.

Kama ilivyotokea katika usitishaji mapigano ya awali, kulikuwa na ripoti kuwa pande zote mbili kukiuka makubaliano hayo.

Jumanne jioni, pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kutokana na moto mkubwa uliounguza makao makuu ya kijasusi, ambayo yapo katika kambi ya ulinzi katikati ya jiji la Khartoum ambayo imekuwa ikipiganiwa tangu mapigano yalipozuka Aprili 15.
Saudi Arabia na Marekani zilisema kwamba iwapo pande zinazozozana zitashindwa kuzingatia usitishaji mapigano watafikiria kuahirisha mazungumzo ya Jeddah, ambayo wakosoaji wamekuwa wakihoji kuwa hayazai matunda.

Chanzo cha habari za taarifa hii zinatoka shirika la habari la Reuters and AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG