Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:59

Sherehe za Eid al-Adha zakosa Shamrashamra Sudan


Wanajeshi na vyombo vya usalama wakati wa swala ya Eid Al-Adha huko Gedaref mashariki mwa Sudan, terehe 28 Juni 2023. Picha na AFP.
Wanajeshi na vyombo vya usalama wakati wa swala ya Eid Al-Adha huko Gedaref mashariki mwa Sudan, terehe 28 Juni 2023. Picha na AFP.

Waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote wanasherekea sikukuu ya Eid al-Adha, kwa wakazi wa jiji la Khartoum sherehe hii imejaa huzuni na haina shamra shamra za kawaida kutokana na mashambulizi yanayoendelea kati ya makundi yaliyohasimiana.

Mawaheb Omar, mama wa watoto wanne ambaye amekataa kuiacha nyumba yake, aliiambia AFP kwamba Eid, ambayo kwa kawaida ni tukio kubwa nchini Sudan, itakuwa "ya huzuni na isiyo na ladha," kwani hawezi hata kununua kondoo, kama sehemu ya kawaida ya mlo wa siku hiyo ya EID.

Mapigano yalipamba moto katika mji mkuu wa Sudan siku ya Jumanne ambao ilikuwa ni ya mkesha wa sikukuu ya Waislamu ya Eid al-Adha, baada ya wanamgambo kukiteka kituo kikuu cha polisi kilichopo katika jiji la Khartoum.

Mapigano hayo katika mji huo ya kati ya jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Burhan na Kikosi cha Msaada wa dharura cha (RSF) kinachoongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, sasa yamejikita katika kambi za kijeshi.

Wakati huo huo katika eneo la magharibi mwa Sudan, huko Darfur mzozo unazidi kuwa mbaya na kufikia "kiwango cha kutisha", Umoja wa Mataifa ulionya.

Tangu kuzuka kwa tarehe 15 Aprili, RSF imeanzisha kambi katika vitongoji vya makazi ya watu katika mji mkuu wakati jeshi likifanya jitihada za kuongeza nguvu ardini licha ya ubora wake wa anga.

Wakati RSF ikipigania kuiteka Khartoum yote, mamilioni ya watu bado wako mafichoni licha ukosefu wa umeme na maji joto kali wakati wa mapigano.

Jumapili jioni, RSF ilisema kuwa imeyateka makao makuu ya polisi yaliyoko kwenye ukingo wa kusini mwa Khartoum, mwaka jana makao hayo makuu ya polisi yaliwekewa vikwazo na Washington kwa ukiukaji wa haki.

Siku ya Jumanne RSF ilishambulia kambi za jeshi zilizopo katikati, kaskazini na kusini mwa Khartoum, mashuhuda walisema.

Chanzo cha habari za taarifa hii zinatoka shirika la habari la Reuters and AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG