Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:39

Mahujaji wawasili kwenye Mlima Arafat siku ya tatu ya Hajj


Mahujaji wasoma dua juu ya Mlima Arafat, Saudi Arabia unaofahamika pia kama Jabal al-Rahma owakati wa kilele cha Hajj, Juni 27, 2023.
Mahujaji wasoma dua juu ya Mlima Arafat, Saudi Arabia unaofahamika pia kama Jabal al-Rahma owakati wa kilele cha Hajj, Juni 27, 2023.

Karibu mahujaji milioni mbili wamewasili mlima Arafat, kuanzia alfajiri Jumanne, ikiwa ndio kilele cha ibada ya Hajj, ikiwa ni idadi ndogo kuliko vile serikali ya Saudi Arabia ilivyotarajia baada ya kuoindolewa masharti yaliyowekwa tangu janga la COVID.

Hajj ya mwaka huu inafanyika wakati wa majira ya joto na watabiri wa hali ya hewa huko Saudi Arabia, wanasema kpimo cha juu cha joto kimefikia nyuzi 46 Sentigredi kati ya saa sita mchana hadi saa tisa.

Huo ni wakati ambao Saudi Arabia imepiga marufuku kwa watu kaufanya kazi wakati wa majira ya joto. Hata hivyo maafisa wa Afya wanasema maelfu ya wafanayakazi wa huduma ya afya wamewekwa tayari ili kuwasadia wale ambao wanaweza kukabiliwa na matatizo ya afya kutokana na joto kali mnamo siku tano za Hajj.

Siku ya Jumanne huko Arafat ambako ina aminika Mtume Mohamed alitoa hutba yake ya mwisho, imekua ni desturi kwa hutba kama hiyo kutolewa siku hii, huku waumini pia wakiomba toba.

Baadhi ya walofika hapo wamewaambia waandishi habari wa mashirika ya kimataifa kuwa wana mchanganyiko wa hisia wakiomba amani kupatikana duniani kama vile huko Sudan, Yemen na Palestina.

Abdulrahman Al-Sherrif kutoka Sudan, ameliambia shirika la habari la AP kwamba anamchanganyiko wa hisia.

"Upande mmoja ninafuraha kuweza kufanya Hajj mwaka huu, lakini pia nina usikitifu mkubwa kutokana na kwamba raia wenzangu wanauliwa kila usiku katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan. Ninawaombea kila la kheri Wasudan na Inshallah Mweneyzi Mungu atarudisha utulivu nchini humo," amesema Al-Sherrif.

Baada ya Arafat, mahujaji wakati wa magharibi wametembea safari fupi hadi Muzdalifa, mahala iliyoko kati kati ya Mlima Arafat na mji wa Mina ambako wanalala nje kwenye uwanja mkubwa. Mahala ambako asubuhi watakusanya vijiwe vidogo na kurusha kwenye maeneo matatu, ikiwa ni tukio la kumrushia shetani ili waepukane na maasi wanaporudi.

Siku hiyo ya Jumatano, ndio wana sherehekea Eid al-Adha ambapo mahujaji na waislamu kote duniani wenye uwezo, wanachinja kondo, ikiwa ni kitendo cha kukumbuka Mtume Ibrahim alipoamrishwa na Mwenyzi Mungu kumtoa mhanga mtoto wake wa kiume Ismael, na alipokua anataka kutekeleza kitendo mtoto aliondoka na kukakuwepo na kondo.

Huu ni wakati wa furaha kubwa kwa wngi walofanikiwa kuwasili na kutekeleza ibada hii muhimu kwa waislamu kama anavyosema Samaher al Faisal kutoka Syria.

"Nina furaha kupita kiasi kuweza kuhiji nina mshukuru mwenyezi mungu. Hatutaki kuondoka hapa Mashallah. Angalia watu wote hapa wakitekeleza Hajj kwa utulivu na Amani," amesema al-Faisal.

Maafisa wa usalama wa Saudi Arabia wanasema kuna wageni milioni 1.8 walofika mwaka huu wakiungana na maelfu ya Wasaudia.

Luteni Kanali Ahmed Sharaf msemaji wa Kituo cha Kitaifa cha Usalama anasema, usalama umeimarishwa zaidi mwaka huu kutokana na mifumo mipya ya kisasa ya usalama inayotumia tenkolojia ya hali ya juu, kufuatilia kila kinachotokea na kuweza kujibu mahitaji yanayowafiki kwa simu katika kipindi cha sekunde 45.

"Tuna mifumo ya kisasa ya teknolojia ya hali ya juu, na vile vile tuna kamera ambazo zimewekwa kwenye vituo vyote takatifu na mskiti mkuu ambapo tunafuatilia kwa karibu kabisa kila kitu kinachotokea na kunawasilisha habari kwa maafisa husika pindi kuna jambo linahitaji kushughulikikwa mara moja," amesema Sharaf.

Baada ya sikukuu ya Eid waumini wanarudi Meccak kuzunguka Kaaba kwa mara ya mwisho kabla ya kukamilisha ibada yote, ambayo ni nguzo ya tano ya Uislamu. Kila mumini anahitajiwa kutekeleza ikiwa ana uwezo wa kifedha na afya nzuri.

Katika kipindi cha Covid watu wenye umri zaidi ya miaka 65 hawakuruhusiwa kwenda kufanya Hija lakini amri hiyo imeondolewa mwaka huu, jambo lililowafurahisha watu wengi kote dunaini.

Mahujaji wawasili Mlima Arafat siku ya tatu ya Hija
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:54 0:00

Forum

XS
SM
MD
LG