Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 18:16

Waziri wa Mafuta wa Iran atembelea kituo muhimu huku hofu ya uwezekano wa shambulizi la Israel ikitanda


Waziri wa Mafuta wa Iran Mohsen Paknejad (Kulia).
Waziri wa Mafuta wa Iran Mohsen Paknejad (Kulia).

Waziri wa Mafuta wa Iran alitua kwenye Kisiwa cha Kharg, katika  kituo kikuu cha usafirishaji wa bidhaa hiyo kwenda nje ya nchi, na kufanya mazungumzo na kamanda wa jeshi la majini Jumapili, tovuti ya habari ya wizara ya mafuta Shana iliripoti.

Hayo yamejiri huku kukiwa na wasiwasi kwamba Israel huenda ikashambulia miundombinu ya nishati katika nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Israel alisema Jumamosi kwamba Israel itajibu shambulio la makombora la wiki iliyopita lililotekelezwa na Tehran, “kwa wakati mwafaka.”

Tovuti ya habari ya Marekani Axios ilinukuu maafisa wa Israel wakisema kwamba vituo vya mafuta vya Iran vinaweza kushambuliwa, wakati Rais wa Marekani Joe Biden alisema Ijumaa kwamba hakudhani Israel ilikuwa imeamua jinsi ya kujibu.

Waziri wa Mafuta Mohsen Paknejad aliwasili Jumapili "kutembelea vituo vya mafuta na kukutana na wafanyikazi wanaofanya kazi katika Kisiwa cha Kharg," Shana iliripoti, ikiongeza kuwa kituo cha mafuta huko kina uwezo wa kuhifadhi mapipa milioni 23 ya ghafi.

Iran ni mwanachama wa Shirika la Nchi Zinazouza Mafuta (OPEC) na huzalisha takriban mapipa milioni 3.2 ya mafuta kwa siku, ambayo ni sawa na asilimia 3 ya uzalishaji wa kimataifa. Uuzaji wa mafuta wa Iran umeongezeka mwaka huu hadi karibu viwango vya juu, vya miaka mingi, vya mapipa milioni 1.7 kwa siku licha ya vikwazo vya Marekani.

Sehemu kubwa ya utajiri wake wa mafuta na gesi iko kusini mwa nchi, ambako kituo cha Kisiwa cha Kharg kipo na ambako karibu 90% ya uuzaji wa mafuta wa Iran unafanyika.

Forum

XS
SM
MD
LG