Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 20:24

Israel imeongeza mashambulizi dhidi ya Hezbollah, Iran imeapa kulipiza kifo cha kamanda


Kiongozi wa kundi la Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah killed
Kiongozi wa kundi la Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah killed

Israel imeendelea kushambulia sehemu toafuti dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon baada ya kuawa kwa kiongozi wa kundi hilo Seyyed Hassan Nasrallah.

Makamanda wengine kadhaa wa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran wameuawa katika mashambulizi ya Israel.

Mashambulizi hayo ni pigo kubwa kwa kundi la Hezbollah, baada ya majibizano ya silaha mpakani kwa karibu mwaka mzima, ambayo yamepelekea viongozi kadhaa wa Hezbollah kuuawa.

Jeshi la Israel limesema kwamba naibu kamanda wa Hezbollah Nabil Kaouk pia ameuawa.

Kundi la Hezbollah lilikuwa halijatoa taarifa kufikia wakati tunaandaa ripoti hii.

Maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Hezbollah wakiwemo waanzilishi wake ambao wamehepa kuuawa au kukamatwa kwa miongo kadhaa, na waliokuwa karibu na Nasrallah, wameuawa.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba Iran imesema kwamba italipiza kisasi kutokana na kifo cha Nasrallah huku kundi la Hezbollah likuwa limeongeza mashambulizi ya roketi kuelekea Israel.

Israel inapambana na waasi Yemen

Israel imetekeleza mashambulizi dhidi ya malengo ya Wahouthi nchini Yemen, baada ya wanamgambo hao kurusha makombora kuelekea Israel katika muda wa siku mbili zilizopita.

Makabiliano hayo yameanzisha vita vingine mashariki ya kati.

Jeshi la Israel limesema katika taarifa kwamba darzeni ya ndege zikiwemo za kivita zimeshambulia mfumo wake wa nshati na dhidi ya bandari za Ras Issa na Hodeidah.

Mashambulizi yamesababisha ukosefu wa umeme katika sehemu kadhaa za bandari ya Hodeida.

Wanamgambo wa kihouthi wamerusha makombora na ndege zisizokuwa na rubani mara kadhaa dhidi ya Israel wakisema ni kuonyesha mshikamano na wapalestina tangu vita vya Gaza vilipoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel Oktoba 7.

Wapiganaji wa Kihouthi wamesema kwamba wamerusha kombora la masafa marefu kuelekea uwanja wa kimataifa wa Ben Gurion karibu na mji wa Tel Aviv, ambalo Israel imesema imelinasa.

Israel pia imesema imenasa kombora lingine Ijumaa.

Marekani imeimarisha jeshi lake mashariki ya kati

Jeshi la Marekani limesema kwamba linaongeza nguvu zake mashariki ya kati na kuwatayarisha wanajeshi wake kwenda eneo hilo huku likionya kwamba Iran inaweza kueneza vita vinavyoendelea.

Tangazo hilo limejiri siku mbili baada ya rais Joe Biden kuielekeza Pentagon kufanya mabadiliko ya jeshi la Marekani katika mashariki ya kati wakati hali ya wasiwasi ikiongezeka kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran. Kuna hofu kwamba Iran inaweza kulipiza kizasi.

Msemaji wa Penatagon Meja Generali Patrick Ryder amesema kwamba Marekani inahakikisha kwamba Iran na washirika wake hawaenezi vita.

Ameonya kwamba iwapo Iran au makundi yanayoungwa mkono na Tehran yatatumia fursa hiyo kulenga wanajeshi wa Marekani au maslahi ya Marekani mashariki ya kati, Marekani itachukua hatua zinazohitajika kulinda watu wake.

Forum

XS
SM
MD
LG