Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 21:25

Hezbollah yasema wapiganaji wake wamekabiliana na wanajeshi wa Israel katika eneo la mpaka wa kusini mwa Lebanon


Watu wakitazama uharibifu wa nyumba kufuatia shambulio la roketi kutoka Lebanon, huku kukiwa na uhasama wa mpaka kati ya Hezbollah na Israel, huko Deir al-Asad, kaskazini mwa Israel, Oktoba 5, 2024. REUTERS.
Watu wakitazama uharibifu wa nyumba kufuatia shambulio la roketi kutoka Lebanon, huku kukiwa na uhasama wa mpaka kati ya Hezbollah na Israel, huko Deir al-Asad, kaskazini mwa Israel, Oktoba 5, 2024. REUTERS.

Hezbollah imesema Jumamosi kuwa  wapiganaji wake walikuwa wakikabiliana na wanajeshi wa Israel katika eneo la mpaka wa kusini mwa Lebanon

Hezbollah imesema Jumamosi kuwa wapiganaji wake walikuwa wakikabiliana na wanajeshi wa Israel katika eneo la mpaka wa kusini mwa Lebanon, ambapo jeshi la Israel lilisema liliwashambulia wanamgambo hao wa vuguvugu linaloungwa mkono na Iran kwenye msikiti mmoja.

Ghasia zinazoongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni zilishuhudia mashambulizi makali ya Israel kwenye ngome za Hezbollah kote Lebanon huku askari wa nchi kavu wakifanya uvamizi karibu na mpaka na kubadilisha karibu mwaka mmoja wa makabiliano ya mpakani kuwa vita kamili.

Katika shambulio la kwanza la anga lililoripotiwa na Israel katika mkoa wa kaskazini wa Tripoli katika mzozo wa sasa kundi hilo la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas limesema mashambulizi ya Wazayuni katika kambi ya wakimbizi ya Beddawi yalimuua kamanda, Saeed Attallah Ali pamoja na mkewe na binti zake wawili Jumamosi.

Forum

XS
SM
MD
LG