Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 05:18

Mkuu wa jeshi la Israel awaomba wanajeshi kujianda kuivamia Lebanon


Picha hii inaonyesha mkuu wa jeshi la Israel, Jenerali Herzi Halevi akimsikiliza afisa. Picha ya Reuters
Picha hii inaonyesha mkuu wa jeshi la Israel, Jenerali Herzi Halevi akimsikiliza afisa. Picha ya Reuters

Mkuu wa jeshi la Israel Jumatano aliwaambia wanajeshi kujianda kwa ajili ya vita vya ardhini kuivamia Lebanon, huku ndege za kivita za Israel zikishambulia kwa mabomu ngome za Hezbollah kwa siku ya tatu mfululizo.

“Mnaweza kusikia milio ya ndege hapa. Tumeshambulia siku nzima, kwa hiyo nikujianda kwa ajili ya vita vya ardhini na uwezekano wenu wa kuingia lakini pia kuendelea kuishambulia Hezbollah,” Luteni Jenerali Herzi Halevi aliwambia wanajeshi wa kikosi cha vifaru, kulingana na taarifa iliyotolewa na jeshi.

“Hatusitishi. Tunaendelea kushambulia na kuwahujumu kila mahali,” Halevi alisema.

Mkuu huyo wa jeshi alizungumza na wanajeshi saa chache baada ya Hezbollah kurusha kombora la masafa marefu ikilenga makao makuu ya idara ya ujasusi ya Israel (Mossad) karibu na Tel Aviv.

Israel iliangusha kombora hilo, lakini Halevi alionya, akisema “Leo Hezbollah imechochea moto, na baadaye leo, watapata jibu lenye nguvu kubwa. Jiandaeni.”

Israel ilisema pia kwamba imewaanda wanajeshi wa akiba ili kupambana na wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.

Maafisa wa afya wa Lebanon walisema mashambulizi ya Israel yaliua watu wengine 50 Jumatano, na kufanya idadi ya vifo kufikia 615 katika siku tatu, huku wengine zaidi ya 2,000 wakijeruhiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG