Masaa kadhaa kabla ya kura kuanza kupigwa, milipuko ilisikika katika upande wa kaskazini mashariki wa mji wa Maiduguri nchini NIgeria.
Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa chanzo cha milipuko hiyo hakikuweza kufahamika mara moja, lakini Boko Haram wametoa taarifa walikuwa wanahusika na shambulizi hilo huko Maiduguri.
Katika mji mwengine kaskazini mashariki wa Geidam, shirika la habari la Reuters limeripoti shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa Kiislam lilosababisha familia kukimbia makazi yao.
Mkazi mmoja wa eneo hilo, akizungumza na Reuters kwa simu amesema, "Tumekimbia, pamoja na wake zetu na watoto wetu na mamia ya watu wengine." Amesema, " Hivi sasa tunakimbia na kujificha maporini."
Rais wa Nigeria anasema vituo vya kupigia kura vitakuwa salama Jumamosi na nchi nzima uchaguzi mkuu unafanyika baada ya kuahirishwa kwa wiki moja.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.