Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:13

Mitizamo mbalimbali juu ya kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu Nigeria


Wagombea Atiku Abubakar (kulia) Mohammadu Buhari
Wagombea Atiku Abubakar (kulia) Mohammadu Buhari

Wananchi wa Nigeria watajitokeza siku ya Jumamosi kupiga kura kumchagua rais na wabunge katika nchi iliyokuwa na idadi kubwa zaidi ya watu, na watarejea tena kwenye vituo vya kupiga kura baada ya wiki mbili kuchagua magavana na wawakilishi wao.

Wapiga kura katika taifa hilo la Afrika Magharibi lazima waamue iwapo watampa fursa tena Rais Muhammadu Buhari kuongoza awamu ya pili.

Kiongozi huyo mstaafu wa jeshi mwenye umri wa miaka 76 alishinda mwaka 2015, kwa ahadi ya kuboresha uchumi wa mafuta ambao Nigeria inautegemea, kupambana na ufisadi na kuzuia hali ya kukosekana amani – hasa upande wa kaskazini mashariki ambako kumeathiriwa zaidi na kikundi cha waislam wenye siasa kali.

Mpinzani mkuu wa Buhari- katika kinyang’anyiro hicho chenye wagombea 60 – ni Atiku Abubakar, mfanyabiashara mwenye miaka 72 na makamu wa rais mstaafu ambaye anafanya kampeni yenye ajenda zinazofanana na mpinzani wake.

Lakini suala jingine linalojitokeza katika uchaguzi : ni uvunjifu wa amani unaohusiana na uchaguzi. Siku ya Jumapili iliyopita peke yake, watu watano walipigwa risasi karibu na mji ulioko kusini mashariki, Warri, katika kile msemaji wa polisi wa eneo hilo amehusisha tukio hilo na mgawanyiko wa kisiasa unaoendelea Nigeria, Shirika la habari la AFP limeripoti.

Shambulizi hilo la kutumia bunduki lilifuatia ugomvi uliyotokea kati ya wafuasi wa chama cha Buhari APC na chama kikuu cha upinzani People’s Democratic Party kinachoongozwa na Abubakar.

“Uvunjifu wa amani ni moja ya tatizo la kila chaguzi,” amesema Patricia Onoja, muuguzi mstaafu mwenye umri wa miaka 60 huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria. Ameiambia Sauti ya Amerika - VOA anawapa ushauri nasaha vijana kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani na ukatili – juhudi ambayo inafanywa pia na makundi mengine ya malezi ya wazazi wa Nigeria.

Kikundi kinachofuatilia haki za binadamu Human Rights Watch kimesisitiza kuwa zaidi ya watu 800 walikufa kutokana na fujo zilizokuwepo wakati wa uchaguzi. Lakini upigaji kura 2015 ulileta makabidhiano ya madaraka baina ya Goodluck Jonathan na Buhari kwa wastani kwa njia ya amani.

Hivi sasa, Nigeria itakuwa inapimwa iwapo “itaweza kufanya chaguzi mbili mfululizo kwa mafanikio na utulivu,” amesema Oge Onubogu, Afisa wa program ya Afrika mzaliwa wa Nigeria anayefanya kazi na Taasisi ya amani ya Marekani ambaye anafuatilia uchaguzi huo kwa karibu sana.

Tume huru ya taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo (NEC) imesema iko tayari kuendesha uchaguzi Jumamosi, pamoja na kuwepo matatizo mbalimbali kama vile kitendo cha hujma kinachoshukiwa cha uchomaji moto jengo jingine la tume lilioko katikati ya jiji la Jos.

Usalama

Buhari, alipohojiwa ikulu, Abuja na VOA mwisho wa mwezi Disemba, amesema vikosi vya usalama vya Nigeria vilikuwa vimepata mafanikio kurejesha sehemu kubwa iliyokuwa inashikiliwa na kikundi chenye msimamo mkali cha Boko Haram kilichoko upande wa kaskazini mashariki ya nchi hiyo.

“Hivi sasa unaweza kuona upande wa kaskazini mashariki Boko Haram haimiliki serikali yoyote ya mtaa katika eneo hilo,” amesema.

Lakini muongo moja uliyopita baada ya kundi la wapiganaji wa Boko Haram kujitokeza walikuwa wamewateka mamia ya watu – na hasa wasichana wa shule huko mji wa Chibok, wengi kati yao bado hawajulikani waliko. Pia wameuwa maelfu na kusababisha mamilioni ya watu kukimbia maeneo yao.

Hivi sasa kikundi kingine kimejitokeza, kinachojulikana kama the Islamic State West Africa Province, imeongezea kutetereka kwa hali ya amani.

Tishio jingine linatokana na kuongezeka kwa migogoro kati ya wachungaji na wakulima kutokana na matumizi ya ardhi katika eneo linalojulinana kama Middle Belt. Kikundi cha kimataifa kinachoshughulikia migogoro kimeripoti zaidi ya vifo 1,300 vinavyohusishwa na mgogoro huo tangu Januari 2018.

Abubakar amekuwa akiulaumu uongozi wa Buhari kwa kile alichokiita ni kushindwa utawala huo kuzuia hali ya kukosekana usalama iliyovuka kiwango nchini Nigeria. Buhari alipochukuwa madaraka hali hiyo ilikuwa tu upande wa kaskazini mashariki” lakini leo hali hiyo imeenea maeneo mengine.

John Campbell, balozi wa zamani wa Marekani nchini Nigeria na mtafiti wa ngazi ya juu katika Baraza la Mahusiano ya Kigeni, ni mhariri wa Ripoti inayofuatilia usalama wa Nigeria. Ripoti hiyo inaonyesha uvunjifu wa amani ulioko maeneo mbalimbali nchini humo.

Anasema anaona “hakuna wazo jipya kutoka kwa wagombea wote wawili kuonyesha namna ya kukabiliana na Boko Haram, hakuna uhalisi wa mazungumzo juu ya njia pana zaidi ya kukabiliana na ukosefu wa usalama jambo linaloathiri nchi nzima.”

Uchumi

Pamoja na kuwa Nigeria ni nchi yenye utajiri wa mafuta na uchumi unaoongoza katika Afrika, bado inaendelea kujikwamua kufuatia kuanguka kwa bei ya mafuta ghafi mwaka 2014. Umaskini umeenea katika nchi yenye watu milioni 200, na inakadiriwa watu milioni 87 (asilimia 44) ambao wameemewa na umaskini, kwa mujibu wa ripoti ya World Poverty Clock.

Katika mahojiano yaliyofanywa na Gallup World Poll nchini Nigeria mwaka 2018, waligundua kuwa kuna ukosefu mkubwa wa chakula cha akiba kwa miaka 13. Watu watatu kati ya watano waliohojiwa – asilimia 71 – wamesema hawana kipato cha kuwawezesha kununua chakula katika baadhi ya nyakati kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Buhari amesema kuwa, iwapo atapewa fursa ya kuongoza awamu ya pili ataangazia katika kuboresha fursa za ajira na kukamilisha miradi ya miundombinu.

Abubakar- ambaye alifanya kazi katika idara ya forodha na sekta ya mafuta na kuasisi chuo kikuu cha American University of Nigeria – anasema anaumahiri mkubwa wa biashara utakaosaidia kujenga uchumi na kutengeneza ajira.

Katika mahojiano na VOA mwezi Januari jijini Washington, Abubakar ameukejeli uongozi wa Buhari juu ya kushuka kwa kiwango cha ajira. Ukosefu wa ajira umeongezeka kwa asilimia 23 mwaka 2018.

Hiyo inamaanisha kuwa zaidi ya watu milioni 20 hawana ajira. “Sio mashara kuwa na ukosefu wa ajira milioni 20,” amesema. “ NI hatari kwa taifa.”

Ni suala muhimu kutengeneza nafasi za ajira, na hasa ikizingatiwa idadi kubwa ya vijana wa Nigeria ambao hawajaajiriwa.

Obadiah Tohomdet, mshauri wa mawasiliano mwenye umri wa miaka 63 Jijini Abuja, amesema mtoto wake alihitimu kutoka katika chuo kikuu miaka mitano iliyopita na mpaka sasa hajaweza kupata kazi isipokuwa vibarua.

Ufisadi

Wafuasi wa Buhari wanasema “yeye sio fisadi.” Lakini wakosoaji wanawashutumu maafisa wa jeshi la Nigeria kwa ufisadi na wanasema uongozi wa Buhari umefumbia macho suala hilo.

Mwezi Januari, rais pia alikosolewa – ndani na nje ya nchi – alipomsimamisha kazi Jaji Mkuu wa Nigeria kumuondoa katika wadhifa wake ambao angekuwa na sauti katika kutatua mgogoro wowote wa uchaguzi.

Kesi ya Walter Onnoghen – ambaye alisimamishwa kwa madai ya kutoa taarifa za uongo juu ya mali zake – liko pembeni halijafanyiwa maamuzi.

Abubaka amekuwa anashukiwa kwa muda sasa. Idhaa ya BBC ilieleza katika taarifa ya wasifu wake wiki iliyopita, kwamba alituhumiwa mwaka 2006 ya kuhamisha fedha za umma kwenda kwenye “maslahi ya biashara zake” wakati akitumikia nafasi ya makamu wa rais.

Ripoti ya kamati ndogo ya Baraza la Seneti la Marekani mwaka 2010 ilidai kuwa Abubakar alihusika kutuma “fedha zenye shaka Marekani” kupitia akaunti ya benki ya mke wake Mmarekani.

Alihusishwa na kesi nyingine : Kutiwa hatiani mwakilishi wa Bunge la Marekani kutokana na kupokea rushwa, William Jefferson, Mdemokrat kutoka Louisiana. Akitambuliwa na serikali ya Marekani kama afisa wa mambo ya nje fisadi, Abubakar alizuiwa kuingia nchini Marekani. Lakini hakufunguliwa kesi yoyot

“Hakuna mtu yoyote aliyeleta ushahidi wowote dhidi yangu juu ya tuhuma za ufisadi,” amesema Abubakar wakati akifanya mahojiano makao makuu ya VOA, Washington.

Ziara yake ya Siku mbili mwezi Januari nchini Marekani – kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 12 – iliondoa uzushi uliokuwa umeenea kwamba angekamatwa alipowasili Marekani. Badala yake, mgombea huyo alikutana na baadhi ya wawakilishi wa Bunge la Congress, Wizara ya Mambo ya Nje na Idara ya biashara ya Marekani.

Abubakar aliweza kupata visa ya Marekani baada ya kundi la ushawishi la Marekani kuingilia kati, Shirika la habari la Bloomberg liliripoti wiki iliyopita.

Abubakar pia amesema kuwa atafikiria kuanzisha programu ya msamaha kuwapa moyo wezi wa fedha za umma kuzirudisha kwa hiari yao.

"Kunamaboresho katika uchaguzi"

Wananchi wa Nigeria wanaangalia uchaguzi unaokuja kwa tahadhari lakini katika hali ya kuwa na imani na mchakato huo, kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na taasisi ya Gallup World Poll iliyotolewa wiki iliyopita.

Iligundua kuwa thuluthi moja ya waliohojiwa – asilimia 34, zaidi ya asilimia 13 iliyopatikana katika utafiti wa 2014 – wanaimani na “ukweli wa matokeo ya uchaguzi,” kufuatia kura ya maoni iliyofanyika katikati ya mwaka 2018.

Kwa kulinganisha, asilimia 49 ya waliotoa maoni yao katika nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara mwaka jana katika kura za maoni zilizofanywa na Gallup walieleza wanaimani na chaguzi zao, amesema Jay Loschky, mkurugenzi wa eneo katika nchi za Afrika zenye kutumia lugha ya Kiingereza. Pia amesema kuwa asilimia 37 ya Wamarekani wameeleza kuwa wanaimani na chaguzi za Marekani.

XS
SM
MD
LG