Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:16

Nigeria : Uchaguzi Mkuu waahirishwa kwa wiki moja


Afisa wa polisi akilinda doria wakati wafanyakazi wa tume ya uchaguzi Nigeria wakipakia vifaa vya kupiga kura katika malori ili kuvipeleka katika vituo vya kupiga kura huko Yola, Nigeria, Feb. 15, 2019.
Afisa wa polisi akilinda doria wakati wafanyakazi wa tume ya uchaguzi Nigeria wakipakia vifaa vya kupiga kura katika malori ili kuvipeleka katika vituo vya kupiga kura huko Yola, Nigeria, Feb. 15, 2019.

Tume huru ya uchaguzi nchini Nigeria (INEC) imeahirisha uchaguzi wa rais na wabunge kwa muda wa wiki moja, masaa machache kabla ya vituo vya uchaguzi kufunguliwa.

Mwenyekiti wa INEC Mahmood Yakubu amewaambia waandishi wa habari Jumamosi - saa tano kabla ya vituo vya uchaguzi kufunguliwa- kuwa "uamuzi huu ulikuwa mgumu kuchukuliwa lakini ni muhimu" kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa mafanikio.

Hata hivyo alitoa maelezo machache kuhusu sababu za mabadiliko hayo kufanyika, lakini akasema "haitawezekana kuendelea na uchaguzi kama ilivyopangwa kwa hivi sasa."

Vyombo vya habari vya ndani nchini Nigeria viliripoti kuwa vifaa vya kupigia kura vilikuwa bado havijawasili katika maeneo yote nchini humo.

Afisa wa INEC aliiambia shirika la habari la Reuters kwamba "baadhi ya karatasi za matokeo ya uchaguzi na baadhi ya karatasi za kupigia kura zimeripotiwa kuwa zimepotea."

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG