Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:03

Gavana atoa idadi mpya ya waliouwawa katika mapigano Nigeria


Vyombo vya usalama vikilinda mitaa ya eneo la Plateau, Nigeria, Juni 25, 2018.
Vyombo vya usalama vikilinda mitaa ya eneo la Plateau, Nigeria, Juni 25, 2018.

Gavana wa jimbo la Plateau lilioko eneo la kati Nigeria amepitia tena idadi ya vifo vilivyotokea mwisho wa wiki vilivyotokana na mapigano kati ya Waislam wafugaji walio wengi na Wakristo wanaojishughulisha na kilimo.

Akizungumza na waadishi Jumanne baada ya kukutana na Rais Muhammadu Buhari, Gavana Simon Lalong amesema mapigano hayo “ yamewaacha zaidi ya watu 200 wameuwawa kitendo chenye kuhuzunisha.”

Vyombo vya usalama Jumapili vimesema idadi ya vifo imefikia 86.

Uhasama wa muda mrefu unaotokana na kugombania rasilmali ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima katika eneo linaloitwa "Middle Belt" linaweza kupelekea kuwa hatari zaidi kuliko uasi unaofanywa na wapiganaji wenye siasa kali wa Boko Haram, ambao umeuwa watu wasiopungua 20,000 katika kipindi cha chini ya miaka 10.

Kadhalika inamweka Rais Buhari katika hali ngumu wakati akiwa anaelekea katika kuomba kuchaguliwa tena Mwakani. Buhari aliingia katika madaraka mwaka 2015 kwa ahadi ya kuwa ataleta utulivu katika nchi iliyo na idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.

Eneo kubwa la Nigeria limegawanyika kidini ambapo Waislam wako Kaskazini na Wakristo upande wa Kusini.

Uasi unaotokana na Boko Haram na mabadiliko ya tabia nchi imewalazimisha wafugaji kuhamia kusini wakitafuta maeneo salama ya kulisha mifugo yao, ambayo imezua mapigano yaliochochewa na hisia za kikabila, kidini na kisiasa.

XS
SM
MD
LG