Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:17

Nigeria : Waliouawa katika mashambulizi Kaduna sasa ni zaidi ya 130


Gavana El-Rufai
Gavana El-Rufai

Zaidi ya watu 130 wameuawa katika mashambulizi ya bunduki kaskazini magharibi mwa Nigeria wiki iliyopita, ikiwa ni mara mbili ya idadi ya vifo iliyoripotiwa na gavana wa jimbo la Kaduna.

Baada ya mkutano na viongozi wa usalama mjini Abuja, gavana Nasir El-Rufai, amethibitisha kwamba sio watu 66 walikufa, bali 130.

El-Rufai amekosolewa kwa kutangaza vifo hivyo siku ya ijumaa, masaa machache kabla ya siku ya uchaguzi mkuu, ulioahirishwa hadi Jumamosi.

Miili ya waliouawa ilipatikana katika vijiji nane, katika eneo la Kajuru ambalo limekumbwa na machafuko mabaya kufuatia uhasama wa kidini na kijamii.

Mwakilishi wa jamii ya Adara, walio wengi katika sehemu hiyo, ameambia shirikala habari la AFP kwamba kumekuwepo mashambulizi ya kila mara kutoka kwa jamii ya Fulani ambao ni waislamu, katika mda wa miaka mitatu sasa.

Vyombo vya habari vya Nigeria vimemnukuu mkuu wa polisi wa jimbo la Kaduna akisema kwamba washukiwa kumi na mmoja wamekamatwa.

XS
SM
MD
LG