Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:27

Uchaguzi wa Rais Nigeria 2019 : Buhari aamrisha vyombo vya ulinzi na usalama kutowahurumia watakaovuruga uchaguzi


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema amewaagiza polisi na jeshi “kutomuonea huruma” mtu yeyote anayejaribu kuvuruga uchaguzi wa rais nchini ambao umeahirishwa hadi Jumamosi.

Tume huru ya uchaguzi ya Taifa (INEC) ilitangaza Ijumaa jioni – masaa kadhaa kabla ya vituo vya kupiga kura kufunguliwa kwa wapiga kura milioni 84 waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura – na kutangazwa kwamba uchaguzi utaahirishwa kwa wiki moja.

INEC imesema uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika Jumamosi, wakati uchaguzi wa magavana na baraza la wawakilishi utasogezwa mbele hadi machi 9, vyombo vya habari nchini humo vimeeleza baadhi ya matatizo yaliyokuwepo katika kusambaza vifaa vya uchaguzi katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo la Afrika Magharibi.

Buhari, mwenye umri wa miaka 76, akizungumza Jumatatu katika mkutano wa dharura wa chama chake cha All Progressives Congress (APC) aliishutumu INEC kuwa "haina uwezo" na kumwonya yeyote atakayejaribu kuharibu masanduku ya kupigia kura na vifaa vya uchaguzi.

“Yeyote anayefikiria anaushawishi katika eneo lake kuongoza kikundi cha wahuni au kuiba masanduku au kuvuruga mfumo wa uchaguzi, atafanya hivyo kwa kulipa thamani ya maisha yake,” Rais amesema.

Chama cha APC na chama cha upinzani cha People’s Democratic Party vimekuwa vikituhumiana kwa jaribio la kutaka kuiba kura.

Rais anakabiliwa na changamoto nzito kutoka mgombea wa chama cha upinzani PDP Atiku Abubakar, makamu wa rais wa zamani.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG