Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:11

Uchaguzi wa urais Liberia una mchuano mkali - Tafiti


Kuhisabiwa kwa kura kunakoendelea nchini Liberia
Kuhisabiwa kwa kura kunakoendelea nchini Liberia

Wanaohisabu kura katika nchi ya Liberia, Afrika Magharibi, Jumatano wameendelea na zoezi la kujumlisha kura zilizopigwa kumchagua Makamu wa Rais Joseph Boakai au mchezaji nyota wa mpira wa miguu George Weah, ambaye alijitabiria kushinda baada ya kupigwa kura Jumanne.

Nimefurahi na najua kuwa nitashinda uchaguzi. Sijahusishwa mpaka sasa na kushindwa uchaguzi huu. Ushindi wa leo ni wauhakika na nitashinda tu, amesema mgombea urais wa Liberia Weah.

Weah amesema ushindi wake hauna shaka kwa sababu muungano wake unaumshuhuri katika kinyang’anyiro hicho. Lakini wapinzani wa Weah, umri miaka 51, wanasema kuwa hana uzoefu wa kisaisa wala uongozi.

Wananchi wa Liberia wamepiga kura ya marudio Jumanne kumchagua rais ajaye. Kwa sasa wanangoja kumalizika kwa hatua ya kuhesabu kura ambayo itachukua siku kadhaa.

Wapinzani wa Boakai, umri miaka 73, wanamtuhumu kuwa mchango wake ni mdogo katika nafasi yake akiwa makamu wa rais wa Sirleaf.

Wasimamizi wa kimataifa, akiwemo Rais mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan, walikuwa katika kituo cha kupiga kura wakifuatilia kuhesabiwa kura, ambapo mpaka sasa unaonyesha haukuwa na dosari kubwa.

“ Kwa hivyo lazima mtu mmoja ashinde. Mtu huyo lazima awe Mwananchi wa Liberia. Na atakayeshindwa pia ni mwanachi wa Liberia. Hivyo basi suala siyo kushindwa na kushinda. Ukishinda utasheherekea na unasheherekea kitaifa kwa sababu wewe ni rais wa wananchi wote wa Liberia. Ukishindwa pia unakubali kwa upole,” amesema Rais Jonathan.

Watafiti wa uchaguzi wamesema uchaguzi wa Jumanne unakaribiana mno kuweza kutabiri na matokeo rasmi hayategemewi hadi baada ya siku chache.

Boakai au Weah mmoja kati yao atamrithi Rais Ellen Johnson Sirleaf, ambaye anaachia madaraka baada ya kutumikia kwa miaka 12 kama rais wa kwanza mwanamke Afrika.

XS
SM
MD
LG