Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:07

Wamishonari Wamarekani 17 na familia zao watekwa nyara Haiti


FILE - Ubalozi wa Marekani mjini Port-au-Prince, Haiti, Julai 9, 2021.
FILE - Ubalozi wa Marekani mjini Port-au-Prince, Haiti, Julai 9, 2021.

Wamishonari wa Marekani takriban17 na familia zao, ikiwemo watoto, wametekwa nyara Jumamosi na genge lilioko mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince, gazeti la New York Times limeripoti, likiwanukuu maafisa wa usalama katika eneo hilo.

Utekaji nyara huo umetokea wakati wamishonari hao walikuwa wanaondoka katika nyumba ya yatima katika taifa la Caribbean lililokumbwa na misukosuko, The Times imesema.

Walitekwa nyara kutoka katika basi lililokuwa linaelekea uwanja wa ndege kuwashusha baadhi ya wamishonari hao katika kikundi hicho kabla hawajaendelea na safari kwenda kituo kingine mjini Haiti, imeongeza ripoti hiyo, ikiwanukuu maafisa wa eneo hilo.

Jennifer Viau, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington, amesema kupitia barua pepe “ tunaliangalia suala hili.” Ubalozi wa Marekani Haiti haukujibu ombi la kupata maoni yao.

Msemaji wa polisi ya Haiti amesema alikuwa anatafuta taarifa juu ya suala hilo.
Ripoti hiyo haikutoa maelezo zaidi juu ya wamishonari hao au kanisa lao.

Ongezeko la ghasia za magenge zimesababisha maelfu kuhama makazi yao na kuzuia shughuli za uchumi katika nchi maskini sana katika eneo la Amerika.

Ghasia hizo zilitokea baada ya kuuawa kwa Rais Jovenel Moise mwezi Julai na tetemeko la ardhi lililotokea Agosti na kuua watu zaid ya 2,000.


Chanzo cha Habari hii ni Shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG