Watu wengine 11 waliokolewa na kukimbizwa hospitali kutoka katika msitu uliopo jirani na mji wa Malindi, kwenye pwani ya bahari ya Hindi nchini Kenya, lakini kuna hofu ya kuwepo kwa waathirika wengine zaidi, kulingana na ripoti ya polisi ambayo shirika la habari la AFP iliiona.
Ripoti hiyo Ilisema polisi walipokea habari kuhusu "vifo vya wananchi ambao ni wajinga waliokufa njaa kwa kisingizio cha kutaka kukutana na Yesu baada ya kushawishiwa na mshukiwa, Makenzie Nthenge, ambaye ni kasisi wa Kanisa la Good News International".
Ripoti za vyombo vya habari zilisema Nthenge alikamatwa na kushtakiwa mwezi uliopita kufuatia vifo vya watoto wawili wa kiume ambao imedaiwa walinyimwa chakula na wazazi wao. lakini baadaye wakaachiliwa kwa bondi dhamana ya shilingi 100,000 za Kenya.
Waumini wanne waliofariki bado hawajatambuliwa, wakati wale waliopelekwa hospitali wametajwa kiwa ni wanaume saba na wanawake wanne wakiwa na umri wa kati ya miaka 17 na 49, kulingana na ripoti ya polisi.
Watatu wako katika hali mbaya.
Wachunguzi wanaendelea na msako katika msitu wa Shakahola, kufuatia ripoti ya uwezekano wa kuwepo kwa kaburi la halaiki ambalo huenda wafuasi wengine wa kundi hilo la kidini walizikwa.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters na AFP