Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:57

Ruto asema serikali haiwezi kuchukua mikopo kuwalipa wafanyakazi


KENYA-CABINET-RUTO-politics
KENYA-CABINET-RUTO-politics

Rais wa Kenya, William Ruto  amesema serikali haiwezi kuchukua mikopo kuwalipa mishahara wafanyakazi wa umma hata pale ambapo jumuiya za wafanyakazi zikitishia kuitisha  mgomo kupinga wafanyakazi  kutolipwa mishahara ya mwezi machi.

Rais Ruto amelaumu kucheleweshwa mishahara kunatokana na deni kubwa la umma ambapo baadhi ya mikopo hiyo ikifikia muda wake wa kuanza kulipwa mwezi huu.

Hata hivyo amesema mishahara italipwa kwa kutumia fedha za kodi zilizokusanywa na mamlaka ya mapato.

Jumuiya mbili kubwa za wafanyakazi zimetangaza kugomba wiki hii kama wanachama wao hawatalipwa mishahara. Akizungumza na vyombo vya habari vya ndani jumatatu, mshauri mkuu wa rais wa masuala ya uchumi amesema kwamba mishahara italipwa mwishoni mwa mwezi lakini aliishauri serikali kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma.

Deni la Kenya sasa linafikia asilimia 65 ya mapato ya taifa.

Nchi inahitaji zaidi ya dola milioni 420 kwa mwezi ili kulipa mishahara na malipo ya uzeeni kwa wafanyakazi wa serikali.

Hii inakuja wiki kadhaa baada ya Benki ya Dunia na shirika la Kimataifa la Fedha kutoa maonyo katika nyakati tofauti kwamba nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara zilikuwa zinatumbukia katika mzozo mpya wa madeni, huku nchi nyingi ziko katika hatari ya kukumbwa na tatizo la madeni.

XS
SM
MD
LG