Watu hao walikutwa wamezikwa kwenye msitu wa Shakahola nchini humo baada ya kutakiwa kuacha kula chakula hadi kufa kwa lengo la kumtafuta Mungu.
Nchi hiyo yenye Wakristo wengi imeshangazwa na tukio hilo la kugunduliwa makaburi ya pamoja mwezi uliopita kwenye msitu karibu na bahari ya Hindi katika mji wa mwambao wa malindi.
Paul Ntheng Mackenze aliyejitangaza kuwa ni mchungaji alianzisha Kanisa la New International Church mwaka 2023 na anashutumiwa kwa kurubuni waumini kwa imani potofu alionekana mahakamani huko Malindi.
Chumba kidogo cha mahakama kilijaa ndugu wa waathiriwa wakati Mackenzie alipokuwa anafikishwa mahakamani na nusu dazani za polisi pamoja na washtakiwa wengine nane.
Waendesha mashtaka wamesema watuhumiwa watashitakiwa kwa makosa ya ugaidi kutokana na vifo hivyo.