Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 07:52

Kenya: Mchungaji mwingine akamatwa kwa mauaji ya wafuasi wake


Polisi wa Kenya wakimshindikiza Ezekiel Ombok Odero, kiongozi wa kanisa la New Life Prayer Centre, kwenye makao makuu ya polisi kwa ajili ya uchunguzi kuhusu mauaji ya kijiji cha Shakahola, Aprili 27, 2023
Polisi wa Kenya wakimshindikiza Ezekiel Ombok Odero, kiongozi wa kanisa la New Life Prayer Centre, kwenye makao makuu ya polisi kwa ajili ya uchunguzi kuhusu mauaji ya kijiji cha Shakahola, Aprili 27, 2023

Kenya Alhamisi ilisema kwamba mmoja wa wachungaji mashuhuri nchini humo atakabiliwa na mashtaka kuhusu “mauaji ya halaiki” ya wafuasi wake, siku chache tu baada ya kupatikana kwa miili kadhaa katika makaburi yanayohusishwa na kanisa lingine.

Ezechiel Odero, kiongozi wa kanisa la New Life Prayer Centre and Church, “alikamatwa na anafanyiwa uchunguzi ili kukabiliana na mashtaka ya uhalifu yanayohusiana na mauaji ya halaiki ya wafuasi wake,” waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki alisema katika taarifa.

“Kanisa hilo limefungwa. Zaidi ya watu 103 waliokuwa wamejificha kwenye majengo wameondolewa na watahitajika kutoa taarifa,” waziri Kindiki aliongeza.

Kukamatwa kwa Odero kunatokea sambamba na uchunguzi dhidi ya Paul Mackenzie Nthenge, kiongozi muhubiri wa dhehebu anayeshtumiwa vifo vya zaidi ya watu 100, wengi wao wakiwa watoto katika msitu karibu na mji wa pwani wa Malindi.

Polisi hawakuhusisha kesi hizo mbili, na maafisa hawakutoa maelezo zaidi kuhusu tuhuma dhidi ya Odero na kanisa lake, lenye makao yake makuu katika mji wa Malindi.

XS
SM
MD
LG