Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:46

Kenya: Polisi wapekua msitu kutafuta miili ya wafuasi wa dhehebu linalodaiwa kuwa la udanganyifu

Polisi ikishirikiana na raia yaifukua miili ya wafuasi wa dhehebu linalodaiwa kuwa laudanganyifu katika msitu wa Shakahola, Malindi, Kenya.
Polisi ikishirikiana na raia yaifukua miili ya wafuasi wa dhehebu linalodaiwa kuwa laudanganyifu katika msitu wa Shakahola, Malindi, Kenya.

Polisi imetumia siku kadhaa kupekua katika msitu wa Shakahola karibu na mji wa mwambao wa Malindi baada ya kupokea taarifa ya dhehebu linaloelezewa kuwa la udanganyifu linaloongozwa na Paul Mackenzie Nthenge ambaye aliwataka wafuasi wake kuacha kula hadi wafe njaa wakimtafuta Mungu.

Noordin Haji mkurugenzi wa mashataka ya umma: “Kanuni ya adhabu inaweza isitoshe lakini tutaangalia na kuona kulingana na aina gani ya ushahidi tunaoupata ili kuturuhusu kupeleka mashtaka yanayoendana na uhalifu ambao umetokea hapa, ambao ni wa kutisha. Kwa kuanzia pengine tutazingatia hata kumshitaki mtu huyo kwa uhalifu unaohusiana na ugaidi kama vile itikadi kali.”

Vyanzo vya habari vya polisi vimeiambia AFP jana jioni kuwa idadi ya vifo imefikia 73 wakati watu kadhaa wakiwa wameokolewa na kupelekwa hospitali.

Ugunduzi huo wa kusikitisha umeleta mshtuko kote nchini na kumfanya rais William Ruto kuaahidi kupambana na vuguvugu la dini zisizokubalika kukiwa na hofu kwamba idadi ya watu walioathiriwa inatarajiwa kuongezeka zaidi.

Polisi na wakazi wa eneo wakipakia miili ya watu ambao ni waathirika wa dhehebu linachodaiwa kuwa la udanganyifu. katika kijiji cha Shakahola, karibu na mji wa pwani karibu na Malindi, kusini mashariki ya Kenya, Aprili 23, 2023.

Inaaminika kwamba wafuasi wa kanisa la Good News International wanaweza kuwa bado wamejificha katika msitu wa Shakahola na wako katika hatari ya kifo ikiwa hawatapatikana haraka.

XS
SM
MD
LG