Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:51

Polisi Kenya wamegundua miili ya watu 51 katika kijiji cha Shakahola huko Malindi

Polisi na wakaazi wa kijiji cha Shakahola huko Malindi nchini Kenya wakipakia miili ya waathirika ambao ni waumini wa kanila la Good News International. April 23, 2023.
Polisi na wakaazi wa kijiji cha Shakahola huko Malindi nchini Kenya wakipakia miili ya waathirika ambao ni waumini wa kanila la Good News International. April 23, 2023.

Polisi walisema msako wa eneo la ndani kutoka Malindi ulikuwa ukiendelea sio tu kwa miili hiyo bali kwa uwezekano wa kuwapata manusura wa kundi ambalo mchungaji wake aliripotiwa kuwaambia wafuasi wakae na njaa hadi kufa ili wakutane na Yesu.

Polisi nchini Kenya wameanza tena msako mkali Jumatatu katika msitu mmoja mashariki mwa nchi hiyo ambako miili ya watu 51 wanaoshukiwa kuwa waumini wa dini wenye msimamo wa kipekee imefukuliwa kutoka katika kina kifupi.

Polisi walisema msako wa eneo la ndani kutoka Malindi ulikuwa ukiendelea sio tu kwa miili hiyo bali kwa uwezekano wa kuwapata manusura wa kundi ambalo mchungaji wake aliripotiwa kuwaambia wafuasi wakae na njaa hadi kufa ili wakutane na Yesu.

Uchunguzi kamili umeanzishwa katika Kanisa la Good News International pamoja na kiongozi wake tangu polisi walipovamia msitu wa Shakahola na kugundua miili ya kwanza wiki iliyopita.

Mwishoni mwa wiki darzeni zaidi za maiti zilifukuliwa na eneo la ekari 800 la msitu lilitangaza eneo la uhalifu huku mamlaka zikitaka kuelewa kiwango halisi cha kile kinachoitwa Mauaji ya Msitu wa Shakahola.

Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome anatarajiwa kutembelea eneo hilo Jumatatu mahala ambapo timu zilizojikusanya zimekuwa zikitafuta mashimo zaidi ya mazishi na uwezekano wa manusura wa waumini hao.

XS
SM
MD
LG