Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:50

Mchungaji aliyedai kutibu UKIMWI mbaroni


Mfuasi aliyeokolewa kutoka msituni akisaidiwa na mfanyakazi wa kujitolea, jirani na msitu wa Shakahola huko Malindi terehe 25, Aprili 2023. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.
Mfuasi aliyeokolewa kutoka msituni akisaidiwa na mfanyakazi wa kujitolea, jirani na msitu wa Shakahola huko Malindi terehe 25, Aprili 2023. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.

Kwa wafuasi wake, Ezekiel Ombok Odero ni kiongozi mwenye kipaji cha kiroho ambaye anaweza kutibu ugonjwa wa HIV kwa kutumia "maji matakatifu."

Kwa wanao mpinga, wanamuona kuwa ni zaidi ya tapeli wa hali ya juu anayewawinda maskini nchini Kenya.

Polisi wa Kenya walimkamata Odero siku ya Alhamisi kutokana na "mauaji ya halaiki ya wafuasi wake" na kukifunga kituo chake cha Maombi cha New Life Prayer, siku chache tu baada ya kugunduliwa kwa dazeni za miili iliyohusishwa na kanisa la kiongozi mwingine wa kidini Mackenzie Nthenge.

Akiwa amezaliwa katika maisha ya kimaskini kwenye kisiwa kilichopo katika Ziwa Victoria, magharibi mwa Kenya, Odero alihangaika na shule na kufanya kazi kama mvuvi kabla ya kuhudhuria mafunzo ya kidini miaka 15 iliyopita.

Sasa amekuwa mwinjilisti tajiri anaye vutia umati mkubwa wa watu, kanisa lake liliopo kusini mwa mji wa pwani wa Malindi , linaweza kuingia watu 40,000 likiwa na hoteli kwa ajili ya wafuasi "kutoka sehemu zote ulimwenguni."

Wakati akisafirishwa kutoka makao makuu hayo ya kanisa kwenda makao makuu ya polisi yaliyoko Mombasa kwa ajili ya mahojiano. Odero, alikuwa amevalia vazi lake maalumu jeupe na akiwa ameshika Biblia.

"Watu hukusanyika kanisani kwangu kwa sababu mimi ndiye niliyechaguliwa," aliakiambia kituo cha habari cha NTV mwezi Desemba mwaka jana

Anajulikana kama Mchungaji Ezekiel, anajenga uwanja wa kutua helikopta, mgahawa na shule ya kimataifa kwenye uwanja wake mkubwa wa kanisa.

Odero anadai kuwa nguo chakavu kuwa ni "takatifu" pamoja na maji yanauzwa kwenye mikutano yake mikubwa kwa shilingi 100 za Kenya yanauwezo wa kuponya ugonjwa wowote, ikiwa ni pamoja na UKIMWI.

Anajivunia chaneli yake ya YouTube yenye watumiaji takriban watu 450,000 ikiwa imejaa ushuhuda wa Wakenya wanaodai kuponywa na Odero – kuanzia wagonjwa wa saratani walioponywa kupitia maombi hadi vipofu wanaoweza kuona tena.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP .

XS
SM
MD
LG