Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:20

Waathirika wa vita vya Darfur wanamatumaini Bashir atafikishwa ICC


Rais wa zamani Omar Hassan al-Bashir akiwa ndani ya kizuizi wakati alipofikishwa mahakamani Disemba 14, 2019 akikabiliwa na tuhuma za ufisadi.
Rais wa zamani Omar Hassan al-Bashir akiwa ndani ya kizuizi wakati alipofikishwa mahakamani Disemba 14, 2019 akikabiliwa na tuhuma za ufisadi.

Uamuzi wa Sudan mwezi huu kuwafungulia mashtaka katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) maafisa wa zamani wa nchi hiyo akiwemo rais Omar al-Bashir aliyepinduliwa, umepokelewa vyema na watu wanaoishi katika eneo la Darfur lenye mapigano.

Tuhuma dhidi ya Bashir na maafisa wengine watatu waliokuwa katika serikali yake, ni pamoja na kuhusishwa na mauaji ya halaiki na uhalifu wa vita walioufanya huko Darfur.

Mauaji hayo yalitokea baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka mwaka 2003. Lakini maafisa wa serikali ya Sudan wamegusia kuwa kesi hiyo huenda isisikilizwe The Hague.

Mohamed Eisa alikuwa na umri wa miaka 12 pale wanamgambo waliposhambulia kijiji chake upande wa Mashariki mwa Darfur miaka 10 iliyopita, na baba yake na ndugu zake kuuawa, na kuwalazimisha familia yote kukimbia kuokoa maisha yao.

Kijana huyu amekuwa akiishi katika muongo mmoja upande wa Magharibi ya Sudan kwenye kambi ya Kalma, kambi kubwa kuliko zote katika eneo la Darfur ikiwahifadhi wale waliolazimika kukimbia makazi yao, ikiwa na wakazi takriban nusu milioni.

Kama ilivyo kwa waathirika wengi wa vita katika eneo la Darfur, Eisa anailaumu serikali ya rais wa zamani Omar al-Bashir kuhusika na vita hivyo, ambavyo Umoja wa Mataifa wanasema imesababisha watu takriban 300,000 kuuawa na watu milioni 2.5 kulazimika kuyakimbia makazi yao tangu mwaka 2003.

XS
SM
MD
LG