Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:27

Shughuli zasimama Sudan kutokana na uhaba wa mafuta ya petroli


Ibrahim Elbadawi, waziri wa fedha wa serikali ya mpito ya Sudan alipohojiwa mjini Khartoum, Sudan, Jan. 28, 2020, speaks in an interview in Khartoum, Sudan, Jan. 28, 2020.
Ibrahim Elbadawi, waziri wa fedha wa serikali ya mpito ya Sudan alipohojiwa mjini Khartoum, Sudan, Jan. 28, 2020, speaks in an interview in Khartoum, Sudan, Jan. 28, 2020.

Upungufu mkubwa wa mafuta umesababisha maelfu ya wafanyakazi wa Sudan kushindwa kwenda kazini na badala yake wakingojea katika mistari mirefu ya msongamano wa magari katika vituo vya kujaza mafuta.

Hali hiyo imesababisha serikali ya mpito kuanzisha utaratibu wa kutoa mafuta ili kujaribu kukabiliana na tatizo kubwa la kiuchumi linalotokana na ukosefu wa mafuta ya petroli.

Baadhi ya watu wamekuwa wakisimama kwa siku kadhaa kwenye mistari mirefu ya msongamano wa magari unaofikia takriban kilomita kadhaa tangu kuanza tatizo la upungufu wa mafuta mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kabla ya upungufu wa mafuta kulikuwepo na upungufu wa mkate jambo ambalo limesababisha hali ngumu kwa serikali mpya inayojaribu kuleta mabadiliko na maisha bora baada ya kupinduliwa kwa Omar Al Bashir mwaka 2019.

Maafisa wa serikali wanasema upungufu wa mafuta hivi sasa unatokana na kuharibika kwa bomba la mafuta kutoka kiwanda cha kusafisha mafuta.

Zaidi ya hayo kusambaza mafuta na uagizaji wa bidhaa unakabiliwa na tatizo la upungufu wa fedha za kigeni na usafirishaji.

XS
SM
MD
LG