Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 18:15

Waafrika Kusini wapiga kura


Mpiga kura katika uchaguzi wa Afrika Kusini
Mpiga kura katika uchaguzi wa Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alipiga kura yake Jumatano (Mei 29) katika uchaguzi wa kitaifa ambapo kura za maoni zinaonyesha kwamba chama chake cha African National Congress (ANC) kiko hatarini kupoteza wingi wake bungeni baada ya miaka 30 madarakani.

ANC iimekabiliwa na kashfa na pia hasira za wananchi juu ya uchumi uliokwama, ukosefu wa ajira wa rekodi ya karibu 33% na kukatika kwa umeme mara kwa mara. Idadi ya kura kwa chama hicho imepungua katika kila uchaguzi tangu mwaka 2004.


Iwapo kitashindwa kupata wingi wa viti bungeni, ANC itabidi ifanye makubaliano na vyama vidogo vya upinzani ili kubaki madarakani -jambo lisilo tarajiwa kwa harakati kongwe zaidi za ukombozi barani Afrika.


Wapinzani wakuu ni chama cha Democratic Alliance (DA) na chama cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters (EFF). Matokeo rasmi yanatarajiwa Mei 31.

Chama cha ANC kinakabiliana na dhana kwamba kinaweza kupoteza udhibiti wake wa kisiasa, wa miongo mitatu, huku wapiga kura wakijitokeza kwenye uchaguzi mkuu.

Zaidi ya wapiga kura milioni 27 wamesajiliwa katika uchaguzi ambao, mshindi wake si bayana, tangu chama cha African National Congress (ANC) kuliongoza taifa hilo kutoka kwa utawala wa kibaguzi -- na huku Rais Cyril Ramaphosa akiomba kuchaguliwa tena.

Huku changamoto za upinzani kutoka upande wa kushoto na kulia, ukosefu wa ajira na uhalifu wa viwango vya juu, na kizazi kipya kinachokua bila kumbukumbu ya mapambano dhidi ya utawala wa watu weupe walio wachache, chama tawala kinaweza kuhitaji kugawana madaraka. Baada ya kupiga kura, Ramaphosa alisema: "Sina shaka yoyote moyoni mwangu kwamba watu kwa mara nyingine, wataweka imani yao kwa ANC kuendelea kuongoza nchi hii. "Watu wa SA wataipatia ANC ushindi."

Lakini kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha upinzani nchini humo, John Steenhuisen wa Democratic Alliance, alitabiri kwamba hakuna chama hata kimoja kingeshinda wingi wa moja kwa moja, na hivyo kutoa fursa kwa muungano wake wa vyama vidogo.
Takriban vyama 70 vinashiriki katika uchaguzi ambao utashuhudia Waafrika Kusini wakipigia kura bunge jipya, na mabunge tisa ya majimbo.

Forum

XS
SM
MD
LG