Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:26

Waandishi wajijengea heshima kwa kufichua rushwa Eswatini


Nchini Eswatini, Zweli Martin Dlamini amejijengea heshima kwa kutokuwa na uoga kutangaza vitendo vya rushwa, akitikisa uwanja wa siasa katika taifa hilo kwa ripoti zake za uchunguzi.

Kuanzia ofisi za serikali mpaka sekta ya dawa, Dlamini ambaye ni muanzilishi na mhariri wa Swaziland News ameibua kashfa baada ya kashfa. Lakini ufichuzi wake wa karibuni sana, ulibaini kashfa ya uhaba wa dawa ukiwahusisha viongozi wa juu, huenda ikawa ndiyo mlipuko mkubwa zaidi.

Shutuma za ubadhirifu wa zaidi ya dola milioni 51 fedha za umma, ndani ya Wizara ya Afya na makampuni mengine mawili, Swazipharm na Ava Pharm, yote yanamilikiwa na Kareem Ashraff, balozi mdogo wa Indonesia nchini Eswatini, imepelekea kusambaa kwa uhaba wa dawa katika hospitali za umma.

Matokeo yake, raia wa kawaida kama Dudu Dlamini mwenye umri wa miaka 44, ambaye pia ni mke, na mgonjwa wa kifafa,, ameachwa bila ya dawa muhimu.

“Mimi ni mgonjwa wa kifafa nahitaji dawa. Sikupata nilichokuwa nakitafuta. Wauguzi waliniambia nisali kwasababu huenda nikapata bahati kwamba hali yangu inaweza kuwa nzuri. Nilikuwa hapa mwezi uliopita pia na bado majibu yalikuwa hayo hayo. Niliambiwa niende kwenye duka la dawa, na hata huko kwenye duka walikuwa hawana dawa.” alisema Dlamini.

Dudu alisafiri kwa takriban saa nzima, umbali wa kilometa 53, kutoka kwenye kijiji chake cha Nsingweni kwenda mjini Manzini, akitafuta dawa ambayo huenda ikasaidia kuokoa maisha yake. Hatima yake na wengine wengi kama yeye ndiyo motisha kubwa wa Zweli Martin Dlamini.

Huku timu ya watu watano, ikidai kufichua ushahidi wa rushwa ndani ya serikali.

Ufichuzi wa karibuni wa Zwemart umebainisha kuhusika kwa zaidi ya maafisa nane wa ngazi ya juu serikali, ikiongezea balozi mdogo wa Indonesia nchini Eswatini, ambako akaunti zake za benki zimezuiliwa ukisubiriwa uchunguzi na kesi inayoendelea mahakamani.

Ripoti ya uchunguzi imebainisha ni ubadhirifu. Rushwa, na mgongano wa kimaslahi kama vigezo vikuu kwa kuendelea kwa uhaba wa dawa nchini Eswatini, kuwanyima wagonjwa rasilimali muhimu.

Serikali imekuwa ikichukua hatua za kisheria kuzifikisha kesi mahakamani. Hakuna hata mmoja ambaye ametuhumiwa ametoa maoni yake kuhusu tuhuma hizo ambazo wameshtakiwa.

Fortunate Bhembe, Naibu Mkurugenzi wa Dawa katika Wizara ya Afya, ni mmoja wa watuhumiwa, anayekabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya fedha. Bado haiko bayana kama yeye na wenzake walioshtakiwa pamoja watakanusha shutuma hizo, na majaribio ya VOA kuwahoji watuhumiwa hayajafanikiwa kwa vile kesi bado inaendelea mahakamani.

Zwemart ambaye ni Muanzilishi na Mhariri wa Swaziland News anasema kwamba kufichua uhalifu kama huo kumemfanya alengwe.

“Kuwa mwandishi wa habari, hara mwandishi wa habari za uchunguzi, kunakuja na hatari na changamoto, kama unavyofahamu,” aliongeza.

“Zimeripotiwa sana kuhusu serikali ya Eswatini, akiwemo Mfalme, kwa mateso hasa mimi kwa kuchapisha Makala zenye kukosoa. Lakini kwa kweli, kama wewe ni mwandishi wa habari na umeamua kusimama dhidi ya wale ambao wana nguvu, huenda ukakabiliwa na changamoto kama hizi.”
Mwanaharakati wa siasa Wandile Dludlu, ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti, People's United Democratic Movement amesema ni kazi muhimu ya Zwemart katika kufichua rushwa na kuhamasisha uwazi.

“Katika nchi, ambako ufalme uko juu ya sheria…. hata katika katiba imeandikwa kwamba hawawezi kuwajibishwa, vitendo vyao kamwe haviwezi kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote, iwe ni mahakama au muundo wowote – inakuwa ni kitovu cha rushwa na utovu wa nidhamu ambao umekithiri katika taifa hilo miaka 56 baada ya ukoloni wa Uingereza,” aliongeza Dludlu.

Katika hali ya kutokuwa na uhakika, Zwemart amekaidi kurudi nyuma katika kupigania haki na uwazi nchini Eswatini.

Dlamini amesema “Kinachonipa hamasa mimi kuendelea kufanya kazi yangu kwa kweli ni kwamba nawakilisha sauti za watu. Watu lazima wajulishwe vizuri kuhusu kinachotokea katika nchi yao, ili waweze, kwa kweli, kufanya maamuzi ya msingi, na kwa kweli kuwawajibisha wale waliohusika. Kuchukua msimamo dhidi ya mamlaka ya Eswatini kulingana na misingi ya uwazi na uwajibikaji.”

Zwemart hivi sasa anaishi uhamishoni nchini Afrika Kusini na ameapa kuendelea na mapambano yake dhidi ya rushwa.

Forum

XS
SM
MD
LG