Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:21

Afrika Kusini kupiga kura Jumatano


Picha ya Maktaba: kiongozi wa upinzani wa chama cha Democratic Alliance (DA) cha Afrika Kusini John Steenhuisen, akiwa Johannesburg, on Oktoba 02, 2023.
Picha ya Maktaba: kiongozi wa upinzani wa chama cha Democratic Alliance (DA) cha Afrika Kusini John Steenhuisen, akiwa Johannesburg, on Oktoba 02, 2023.

Maafisa wa uchaguzi wa Afrika Kusini wako kwenye maandalizi ya mwisho kwaajili uchaguzi wa kesho, miaka 30 baada ya nchi hiyo kumaliza utawala wa kibaguzi na huenda ikawa ni mara ya kwanza kwa chama tawala cha muda mrefu cha African National Congress (ANC) kupoteza viti vingi vya wabunge.

Utafiti mwingi wa maoni umetabiri kwamba ANC itapata chini ya asilimia 50 na itakabiliwa na uwezekano wa kupoteza mamlaka kwa mara ya kwanza tangu iliposhinda udhibiti wa serikali iliyoongozwa na Nelson Mandela katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo mwaka 1994.

Katika jimbo la KwaZulu-Natal kamishna wa polisi, Jenerali Nhlanhla Mkhwanazi alisema Jumanne kwamba maafisa wa polisi 17,000 watatumwa katika sehemu mbali mbali za jimbo hilo la Mashariki akisema ni katika kukabiliana na kuongezeka kwa ukosefu wa utulivu wa kisiasa katika maeneo mahususi.

Vituo vya Kura vitafunguliwa hapo saa moja asubuhi, huku matokeo ya awali yakitarajiwa kutolewa katika siku zinazofuata.

Chini ya mfumo wa uchaguzi wa Afrika Kusini, wananchi hupigia kura vyama vya kisiasa, ambavyo hupata viti bungeni kulingana na asilimia ya kura iliyopigwa, na hapo tena wabunge wanamchagua rais.

Forum

XS
SM
MD
LG