Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:20

Matukio mabaya ya hali ya hewa yasababisha milipuko ya kipindupindu Afrika


MAKTABA - Mgonjwa wa kipindupindu akiwa kwenye kitanda cha hospitali huko Harare, Zimbabwe, Novemba . 19, 2023. Picha na AP
MAKTABA - Mgonjwa wa kipindupindu akiwa kwenye kitanda cha hospitali huko Harare, Zimbabwe, Novemba . 19, 2023. Picha na AP

Matukio ya hali mbaya ya hewa yaliyolikumba bara la Afrika katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, na dhoruba za kitropiki, mafuriko na ukame yamesababisha majanga ya njaa ukosefu wa makazi. Na kupelekea tishio jingine baya: ikiwemo milipuko mibaya ya kipindipindu barani humo.

Huko Kusini na Mashariki mwa Afrika, zaidi ya watu 6,000 wamefariki na takribani visa 350,000 vimeripotiwa tangu mfululizo wa milipuko ya kipindipindu ianze mwishoni mwa mwaka 2021.

Malawi na Zambia zilipata milipuko mibaya iliyovunja rekodi, Zimbabwe imekubwa na matukio kadhaa, Kenya, Ethiopia na Somalia pia zimeathiriwa vibaya.

Nchi zote zimekumbwa na mafuriko au ukame — katika baadhi yanyakati, zimekumbwa na matukio yote mawili — na mamlaka za afya , wanasayansi na mashirika ya misaada inasema ongezeko ambalo halikutarajiwa la maambukizi ya bakteria watokanao na maji huko Afrika, mfano mpya kabisa wa jinsi hali mbaya ya hewa inavyochangia ongezeko la milipuko ya majonjwa.

“Milipuko inazidi kuwa mikubwa kwa sababu ya matukio mabaya ya hali ya hewa” alisema Tulio de Oliveira, mwanasayansi aliyoko Afrikia Kusini anayefanya utafiti wa magonjwa katika nchi zinazoendelea duniani.

De Oliveira aliyeongoza timu iliyotambua aina mpya ya virusi vya corona wakati wa janga la COVID-19, alisema milipuko ya hivi karibuni kusini mwa Afrika inaweza kufuatiliwa kwa vimbunga na mafuriko yaliyoikumba Malawi mwishoni mwa 2021 na mwanzoni mwa 2022, vilivyobeba bakteria wa kipindupindu kwenda katika maeneao ambayo si kawaida kufikiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG