Viongozi hao pia walizungumzia hatua zilizochukuliwa na taifa hilo kutokana na mlipuko wa karibuni wa kipindupindu. Zambia inakabiliana na mlipuko mkubwa wa kipindupindu ambao tayari umeua takriban watu 333 tangu Oktoba, wakati maambukizi 8,000 yakiripotiwa tangu wakati huo, kulingana na mtandao wa ubalozi wa Marekani nchini Zambia.
Naibu waziri wa fedha wa Marekani kwa ajili ya masuala ya kimataifa Jay Shambaugh, amezizitiza azma ya Marekani ya kushirikiana na Zambia, katika kuangamiza mlipuko huo, wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na waziri wa Fedha wa Zambia, Situmbeko Musokotwane, taarifa zimeongeza.
Zambia ambayo ni mzalishaji mkubwa zaidi wa Shaba barani Afrika, ilichelewa kulipa madeni yake miaka mitatu iliopita kutokana na janga la Corona, na tangu wakati huo imekuwa ikijikokota kuyalipia.
Forum