Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:24

Milipuko ya magonjwa yakithiri DRC


Mtoto akipata huduma katika kituo cha afya cha Kanyaruchinya Novemba 11, 2022. Picha na AFP
Mtoto akipata huduma katika kituo cha afya cha Kanyaruchinya Novemba 11, 2022. Picha na AFP

Shirika la Afya Ulimwenguni lilitoa tahadhari leo Ijumaa kuhusu hali mbaya ya afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo kipindupindu, surua, kimeta na tauni vinasababisha hatari kubwa ya afya kwa wakazi.

Mgogoro wa kiafya unazidishwa na ghasia, Mabadiliko mabaya hali ya hewa, kufurushwa kwa wakazi, umaskini na utapiamlo, kwa mujibu wa WHO, huku ikitoa wito wa ufadhili kuongezwa haraka.

Boureima Hama Sambo, mwakilishi wa WHO nchini DR Congo anasema Changamoto zinazowakabili watu wa DRC zimefikia viwango vya kutisha.

Akziungumza na waandishi wa Habari huko Geneva kwa njia ya video, Sambo amesema katika maeneo mengi ya DRC, haswa yaliyoko mashariki mwa nchi hiyo, raia wanakabiliwa na mapigano mapya, na hospitali zimejaa watu waliojeruhiwa.

Aidha aliongeza kuwa DRC inakabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu tangu 2017, ikiwa na visa 50,000 zinazoshukiwa na vifo 470 vilirekodiwa mnamo 2023 huku ikipambana na janga kubwa zaidi la surua tangu 2019, na karibu visa 28,000 na vifo 750 hadi sasa mnamo 2024.

Zaidi ya hayo, mlipuko ambao bado unazuka wa ugonjwa wa MPOX, ambao zamani ulijulikana kama Monkey POX, unaongezeka, na karibu kesi 4,000 zinazoshukiwa na vifo 271 kufikia sasa mwaka huu.

Zaidi ya theluthi mbili ya visa hivyo vinaripotiwa kwa watoto. Sambo aliongeza kuwa "Takriban watu milioni 20 wanahitaji usaidizi wa kiafya lakini bado hakuna ufadhili.

Alisema Ulimwengu haupaswi kufumbia macho hali ambayo inaweza kuwa na madhara makubwa kwa usalama na afya katika kanda.

Forum

XS
SM
MD
LG