Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:59

Mapigano DRC yamesababisha mgogoro wa kibinadamu; Inasema IFRC


Nembo ya Chama cha Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC)
Nembo ya Chama cha Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC)

IFRC ilitoa ombi la dharura la dola milioni 57 kuwasaidia kwa haraka watu 500,000 waliokuwa hatarini kukoseshwa makazi

Chama cha Msalaba Mwekundu siku ya Ijumaa kilisema mapigano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha mgogoro mkubwa kuna hatari kuwa hautatambuliwa na kuomba takribani dola milioni 60 kutoa msaada uliohitajika sana.

Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC), mtandao mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani, ulionya kuhusu ongezeko baya la ghasia katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, kwenye mpaka wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

IFRC ilitoa ombi la dharura la dola milioni 57 kuwasaidia kwa haraka watu 500,000 waliokuwa katika hatari kubwa ya kukoseshwa makazi yao pamoja na jamii zao zilizowakaribisha.

Umoja wa Mataifa ulisema Jumatano zaidi ya watu 100,000 walikoseshwa makazi wiki hii, wengi wao kutoka karibu na mji wa Kivu Kaskazini wa Nyanzale, ambako takriban watu 80,000 waliishi huko pamoja na maelfu ambao tayari walikimbia mapigano ya awali katika eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG