Mji wa Harare wenye watu milioni 1.5 umeathiriwa vibaya na mlipuko wa ugonjwa huo ambao umeathiri majimbo yote ya taifa hilo la kusini mwa Afrika.
"Tumetangaza hali ya dharura kwa sababu hali kwa sasa ni mbaya sana," meya wa jiji hilo aliliambia shirika la habari AFP.
"Ugonjwa unaenea kote katika jiji hilo."
Zimbabwe imerekodi kesi zaidi ya 7,000 za watu wanaoshukiwa kuwa na kipindupindu na takriban vifo vya watu 150, ambapo 51 vimethibitishwa na vipimo vya maabara, tangu ugonjwa huo uzuke mwezi Februari.
Takriban watu 12 wamefariki mjini Harare.
Mlipuko wa kipindupindu hutokea mara kwa mara katika miji ya Zimbabwe ambako usambazaji wa maji ya kunywa na huduma za vyoo si za uhakika na miundombinu imeporomoka kutokana na kupuuzwa kwa miaka mingi.
Mlipuko huo ulitokea katika kipindi kibaya cha mzozo wa uchumi wa nchi hiyo wakati hospitali nyingi za umma zilifungwa kwa sababu ya uhaba wa dawa na wafanyakazi wa afya kukimbilia nje ya nchi.
Mapema mwaka huu, Umoja wa Mataifa ulisema Kipindupindu kumeibuka tena duniani tangu 2021 baada ya muongo mmoja wa kuendelea kupungua.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP
Forum