Sullivan alionekana kwenye kituo cha televisheni cha ABC Akizungumzia msimamo wa Marekani katika vita ya Tel Aviv dhidi ya hamas .
“Tunaamini umuhimu wa sheria za vita, maana yake kuchukua kila hatua inayowezekana kuwalinda raia. Wakati huo huo tutaendelea kusimama nyuma ya pendekezo la Israel kwamba Israel ina haki ya kujitetea dhidi ya mashambulizi ya kigaidi.”alisema Sullivan.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye alisisitiza nchi yake itaendelea na operesheni za kijeshi huko Gaza mpaka iishinde Hamas.
Alipohojiwa na kituo cha televisheni cha CNN, siku ya Jumapili, aliombwa atoe maoni yake kuhusu matamshi ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken kwamba Wapalestina wengi wameuawa huko Gaza.
Netanyahu alisema “Nadhani kufariki kwa raia yeyote ni janga. Lawama ni vyema ielekezwe kwa Hamas kwa sababu wanawazuia kuondoka katika eneo la vita mara nyingine kwa mtutu wa bunduki. Wamefanya mashambulizi kwenye maeneo salama na kwenye njia salama ambazo tuliziweka.”
Katika suala tofauti, Netanyahu alizungumzia uvumi kuhusu uwezekano wa makubaliano kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka zaidi ya 240, waliotekwa na Hamas Oktoba 7. Matamshi yake aliyoyatoa kwenye kituo cha televisheni cha NBC katika kipindi cha Meet the Press alisema.
“Kazi isiyo ya kawaida ambayo IDF inaifanya, kuweka shinikizo kwa uongozi wa Hamas. Hicho ni kitu ambacho huenda kikaleta makubaliano na kama makubaliano yapo, ndiyo tutatuzungumza kuhusu hili utakapofika wakati huo. Tutatangaza kama limefanikiwa.”
Waziri Mkuu aliongezea kwamba wakati vita vitakapokwisha, jukumu la jumla kwa jeshi huko Gaza litabaki katika mikono ya Israel, lakini hiyo ni mapema mno kusema nani ataiongoza.
“Kuhusiana na utawala wa kiraia wa Gaza. Tunahitaji kuona mambo mawili. Gaza haina jeshi na Gaza lazima kusiwepo na wenye msimamo mkali. Nadhani mpaka sasa, hatujaona jeshi lolote la Palestina ukijumuisha Mamlaka ya Palestina ambayo ina uwezo wa kufanya hivyo,” alisema waziri mkuu wa Israel.
Wakati huo huo, raia wa Palestina wanaendelea kukimbilia upande wa kaskazini mwa Gaza, wakati mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yanatoa wito wa kusitishwa haraka kwa mashambulizi dhidi ya mahospitali.
Forum