Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:49

Mapigano makali Gaza yasababisha hospitali ya Shifa kushindwa kutoa huduma


Wagonjwa na watu waliopoteza makazi wakiwa katika hospitali ya Al-Shifa huko Gaza Novemba 10, 2023. Picha na AFP
Wagonjwa na watu waliopoteza makazi wakiwa katika hospitali ya Al-Shifa huko Gaza Novemba 10, 2023. Picha na AFP

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema kituo cha matibabu cha Shifa huko Gaza "hakifanyi kazi tena kama hospitali" na hali katika hospitali hiyo kubwa zaidi ya Gaza ni "mbaya na ya hatari."

Mkuu wa WHO alisema, "milio ya risasi na milipuko ya wakati wote" karibu na hospitali "imezidisha hali hiyo ambayo tayari ni mbaya sana ."

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema siku ya Jumapili hakuna sababu ya kushindwa kuwahamisha kwa usalama wagonjwa waliopo katika hospitali hiyo ya Shifa iliyozingirwa huko Gaza, lakini akasema kwamba wanamgambo wa Hamas "wanafanya kila hila kuwaweka hatarini."

Kiongozi huyo wa Israel aliiambia CNN katika kipindi cha “State of the Union” kuwa wagonjwa 100 wametolewa nje ya hospitali na kwamba maelfu ya Wapalestina wanaoishi katika maeneo jirani wameondoka kwa usalama kwenda nje ya eneo hilo wakitumia njia salama kuelekea kusini nje ya Gaza City.

Lakini mapigano kati ya Israel na Hamas yaliendelea katika maeneo jirani na hospitali hiyo kubwa zaidi iliyoko Gaza, na mkurugenzi wa hospitali hiyo, Mohammad Abu Salmiya, alisema kituo hicho kimezingirwa na mzozo huo.

Matibabu kwa baadhi ya wagonjwa katika hospitali hiyo yamesitishwa kwa sababu ya upungufu wa mafuta, huku watoto wawili wamefariki dunia na darzen ya wagonjwa wengine kuachwa hatarini. Netanyahu, bila kutoa maelezo zaidi, alisema Israel "imeipatia mafuta hospitali ya Shifa," lakini "wameyakataa."

Forum

XS
SM
MD
LG